CRIO INTERNATIONAL BIBLE COLLEGE YATOA FURSA YA MAFUNZO YA BIBLIA KWA WATUMISHI
Mkurugenzi wa CRIO International Bible College, Dr. Willy K. Ackyoo, amewakaribisha watumishi wa Mungu na wananchi wote wenye nia ya kujifunza Neno la Mungu kujiunga na chuo hicho kwa ajili ya kupata mafunzo ya Biblia na kujiendeleza katika huduma.
Dr. Ackyoo amesema chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Makao Makuu ya Kanisa la Bethel Calvary Church, kinatoa fursa kwa watumishi wanaohitaji kujijengea uwezo zaidi pamoja na watu wanaotaka kuanza masomo ya Mafunzo ya Biblia.
Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha washiriki kuongeza uelewa wao wa Neno la Mungu, kujenga uwezo katika huduma na kujiandaa kwa majukumu mbalimbali ya uongozi na utumishi wa Kikristo.
Kwa mujibu wa Dr. Ackyoo, CRIO International Bible College kinatoa programu mbalimbali za masomo ikiwemo Mafunzo ya Kina ya Biblia, Mafunzo ya Kitheolojia pamoja na Maandalizi ya Umisionari.
Amesisitiza kuwa watu wote wenye nia ya kujifunza na kuongeza maarifa katika masuala ya Biblia wanakaribishwa kujiunga na chuo hicho, huku akieleza kuwa wale watakaokidhi vigezo na kuhitaji maelezo zaidi wanaweza kuwasiliana na uongozi wa chuo.
Dr. Ackyoo amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za chuo hicho kuwawezesha watu kujenga maisha yao, kuimarisha utume wao, kuelewa Neno la Mungu na kutumia maarifa hayo katika kubadilisha jamii.
Ameongeza kuwa masomo hayo yanaanza rasmi, hivyo watumishi na waumini wenye nia ya kujiendeleza wanashauriwa kuchukua fursa hiyo na kuwasiliana na chuo kwa ajili ya kupata maelekezo ya namna ya kujiunga.
CRIO International Bible College imetangaza kuwa watu wanaohitaji taarifa zaidi kuhusu mafunzo hayo wanaweza kuwasiliana na uongozi kupitia namba 0754 648 158.
Kaulimbiu ya chuo hicho ni: “Jenga maisha yako, imarisha utume wako, elewa Neno, badilisha ulimwengu

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia