BAKHRESA AIPONGEZA TRA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WALIPAKODI

 



Said Salim Bakhresa ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na walipakodi, na kutoa wito wafanyabiashara kuzingatia sheria na kutekeleza wajibu wa kikodi. 

Bakhresa ameyasema hayo leo tarehe 31 Agosti, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamishna wa Idara ya Walipakodi Wakubwa, Bw. Edmund Kawamala, pamoja na Naibu Kamishna Uendeshaji, Bi. Eva Raphael, iliyolenga kusikiliza maoni na changamoto  pamoja na kujadili maeneo ya ushirikiano.

Kwa upande wake, Bw. Kawamala amempongeza Bw. Bakhresa kwa kuendelea kuonesha uwajibikaji katika kutekeleza wajibu wake wa ulipaji kodi



Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za TRA za kuimarisha mawasiliano na walipakodi na kuboresha huduma za kikodi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya pande zote.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia