WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO


 Na Woinde Shizza,Arusha
Kampuni ya TanzaniteOne ya Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro
Mkoani Manyara, imetoa msaada wa vifaa vya mchezo wa soka vya thamani ya
sh5.7 milioni, kwa timu nne zilizoingia nusu fainaliya ligi ya Taifa
daraja la tatu ngazi ya mkoa.


Kaimu Mkurugenzi wa TanzaniteOne Apolinary Modest, akikabidhi juzi msaada
huo kwa Mwenyekiti wa Chama cha soka wilayani Simanjiro Jumanne Mkopi,
alisema wametoa sehemu ya faida kwa jamii ili kunyanyua michezo.


Modest alisema msaada huo wa seti 18 ya jezi za timu nne, suti za viongozi
wa timu, nyavu za magoli, mipira sita na vifaa vya waamuzi, utasaidia
kunyanyua mchezo huo ambao miaka iliyopita ulikuwa maarufu kwa mchezo wa
riadha.


“Manyara imekuwa nyuma kwenye mchezo wa soka kutokana na kuonekana kuwa
ipo pembezoni, hivyo wafadhili kushindwa kujitokeza na kudhamini ila
wajitokeze sasa ili kunyanyua michezo kwani ni ajira, afya na umoja,”
alisema.



Mwenyekiti wa Saidia wana jamii nchini (Sawata)

Mohamed Mughanja ambaye alikuwa kiunganishi cha kampuni ya TanzaniteOne na
SIDFA kwenye kupata msaada huo, alisema kupitia msaada huo vijana
wataongeza morali ya michezo.


“Timu mbili zilizoingia nusu fainali ya soka ligi ya Taifa daraja la tatu
ngazi ya mkoa kwenye vituo viwili vya uwanja wa barafu wa Mirerani wilayani
Simanjiro na Kibaya wilayani Kiteto zitanufaika na msaada huu,” alisema
Mughanja.


Mwenyekiti wa SIDFA, Jumanne Mkopi aliishukuru kampuni ya TanzaniteOne kwa
kutoa msaada huo na aliahidi kuzigawa kwa vilabu vyote vinne ambavyo
vimeingia nusu fainali ya michuao hiyo kwa ngazi ya mkoa wa Manyara.



“Baada ya kuzigawia baadhi ya vifaa hivi kwa timu mbili zilizokuwa hapa
Mirerani nitasafiri kwenda Kibaya wilayani Kiteto ili kuvipa vilabu vingine
viwili vilivyofanikiwa kuingia nusu fainali katika kituo hicho,” alisema
Mkopi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post