Mkuu
mpya wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu
amewaagiza watumishi wasio na sifa za kuajiriwa kujiondoa kabla
ya March 31 mwaka huu.Kijuu alitoa
kauli hiyo jana wakati wa Makabidhiano ya ofisi baina yake na
mkuu wa mkoa wa zamani,John Mongella ambapo alisema kwamba
Tanzania inawatumishi hewa zaidi ya 2000, hivyo ana imani hata
Kagera wapo.
"Hao watumishi hewa endapo watang'ang'ania kubaki katika vitengo walivyopo nitawashughulikia wahusika wakuu wa vitengo hivyo," alisema
Aidha,
aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa
mabaraza ya usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi mkoa ili
kusimamia haki za wananchi.
Pia
aliwataka watumishi wa serikali mkoani humo kufahamu maudhui ya
"Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa na
uadilifu.
Aliwataka
kutosubiri kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina nani na
wanapaswa kufanya nini kutokana na majukumu waliyopewa.
Alisema
ili kufikia lengo la Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi
kwa uaminifu ni lazima kushikiria uadilifu na kutambua kwamba
watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.