WADAU WA ELIMU MKOA WA ARUSHA WAKUTANA; MAANDALIZI YA KIDATO CHA KWANZA 2028
Kampeni ya kuhamasisha Ufadhili wa pamoja kwa Maendeleo ya Elimu Kupitia GPE Multiplier yazinduliwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imekutana na Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu kupitia Kampeni ya kuhamasisha Ufadhili wa pamoja kwa Maendeleo ya Elimu Kupitia GPE Multiplier, Mkoa wa Arusha, ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kiadoto cha kwanza mwaka 2028
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa kampeni hiyo mkoa wa Arusha, leo Novemba 26, 2026, kwa niaba ya Mkuu wa Moa wa Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Luteni Kanali Robert Kakomangile, amewahimiza waadau kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu, ili kukidhi mahitaji ya miundombkuunya shule kwa ajli ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2028 (Double Cohort).
"Kampeni hii ya uchangiaji wa pamoja inatoa fursa kwa wadau kuunganisha nguvu na rasilimali ili kuongeza fedha zitakazopatikana kupitia GPE Multiplier Grant kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya elimu, kwa kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, inatoa firsa kwa wadau kushiriki kuchangia sekta ya elimu na kazi kubwa imefanyika" Amesema Mhe.Luteni Kanali.
Mhe. Luteni Kanali Kakomangilba amewakumbusha wadau hao kuwa, mkoa bado una mahitaji ya miundombinu ya elimu kutokana na matarajio ya mkoa huo kupokea kundi kubwa la wanafunzi wa kidato cha kwanza (Double Cohort) mwaka 2028, jambo linasababisha ongezeko kubwa la mahitaji ya miundombinu na rasilimali za elimu.
"Mkoa wa Arusha utahitaji vyumba 1,317 vya madarasa, matundu 2,410 ya vyoo na maabara 172 ili kumudu idadi kubwa ya wanafunzi kwa mwaka 2028, hivyo, ni muhimu kuanza maandalizi mapema ili kuhakikisha shule zetu zinakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi wote katika mazingira bora na salama".Amesisitiza Mhe. Luteni Kanali Kakomangile,








0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia