𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗔𝗪𝗔𝗢𝗡𝗬𝗔 𝗪𝗔𝗞𝗨𝗨 𝗪𝗔 𝗠𝗜𝗞𝗢𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗜𝗟𝗔𝗬𝗔 𝗪𝗔𝗟𝗜𝗢 𝗪𝗔𝗭𝗘𝗠𝗕𝗘 𝗣𝗔𝗠𝗢𝗝𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗧𝗨𝗠𝗜𝗦𝗛𝗜 𝗪𝗔𝗦𝗜𝗢𝗧𝗨𝗟𝗜𝗔 𝗞𝗔𝗭𝗜𝗡𝗜

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwajibika ipasavyo katika kusimamia watumishi, miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa kufanya majukumu hayo.


Rais Samia ametoa agizo hilo leo, Novemba 27, 2026, Ikulu ya Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule na kusema baadhi ya watendaji wameshindwa kusimamia nidhamu ya watumishi, huku wengine wakiingia kazini na kupotea bila kujulikana walipo.


Aidha, ameeleza kutoridhishwa na usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali, akibainisha kuwa kuna miradi ambayo wakandarasi hulipwa fedha za awali lakini utekelezaji haufikii hata asilimia 10, huku wakirejea kuomba malipo mengine.


Rais Samia pia amesisitiza kuwa jukumu la kusikiliza na kutatua kero za wananchi ni la Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika maeneo yao, akieleza kuwa Waziri Mkuu anapaswa kupumzika majukumu ya kuzunguka kutatua kero hizo na kuelekeza nguvu katika kuratibu shughuli za Serikali kitaifa.


Vilevile, amewataka Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wengine wa Serikali kutangaza na kueleza kwa wananchi mafanikio na miradi inayotekelezwa katika sekta zao ili wananchi wafahamu hatua zilizofikiwa na huduma zinazotolewa na Serikali.


#KaziNaUtuTunasongaMbele

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia