Picha ya pamoja Apostle wa kwanza kushoto,Mhe Makonda,Mke wa Apostle Ndegi ni mke wa Mh. Makonda
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi siku ya jana katika ibada amemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda biblia ya Neno la Mungu kwa makusudi ya kusoma Neno hilo kila siku ili liweze kuwa msaada wake katika shughuli za kila siku za Kiserikali!
Ni siku chache tangu Mh. Rais Magufuri ateue wakuu wa Mikoa nchini,hivyo kwasasa majukumu na upinzani kwake utakuwa mkubwa zaidi na mwanzo,hivyo anamhitaji Mungu sana Alisema Apostle Ndegi.Apostle Ndegi aliongeza kwa kusema Mh. Makonda anahitaji maombi ya kila Mtu kwa Mungu ili afanikishe majukumu yake sawasawa.
Mh.Makonda akiongea alisema kila mtanzania kwa nafasi yake lazima ahakikishe anatimiza majukumu yake vizuri tena kwa kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo kwa nafasi ya mtu mmoja na kuacha kutegemea na kusubiri serikali.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Makonda aliongozana na Mke na Mrisho Mpoto katika Ibada hiyo.
|