
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Geita vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Kasheku Musukuma
Amewahi
kutamka bungeni kuwa vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wanauawa
wanne kwa wiki kitu ambacho ni kibaya na sio cha kibinaadamu.
Mbunge huyo alisema kuwa kutokana na kampuni ya
Msama kutambua umuhimu wake wana kila sababu ya kuwaunga mkono na
angependa kuona wananchi wanajitokeza kwa
wingi katika tamasha hilo ili kuzungumza na Mungu kupitia waimbaji na
viongozi wa dini katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya
ziwa.
Alisema hiyo ni kama dawa ambayo imekuja kutibu
tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu
wa ngozi na vikongwe hivyo anaamini
kuwa nguvu za Tamasha hilo wataweza kusonga
mbele.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama
alisema tamasha hilo litafanyika mkoani Geita kuanzia Machi 26 kwenye
ukumbi wa Desire, Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Machi 28
litafanyika uwanja wa Taifa wilayani Kahama.
Waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.