Shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, Fastjet Tanzania limeongeza
idadi ya safari zake kwenye njia yake ya Dar es Salaam na Nairobi
ikiwa ni mwitikIo mkubwa kwa mahitaji ya abiria.
Kuanzia
Machi 21 fastjet itakuwa inafanya safari zake mara mbili kwa siku
kwenda na kurudi kati ya miji hiyo miwili kila siku ndani ya wiki na
hivyo kufanya safari zake kuwa ni 28 kwa wiki kati ya Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Uwanja wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Shirika
hilo ambalo hadi sasa linafanya safari moja kila siku kati ya miji
hiyo miwili, limeongeza masafa yake ya kuruka ili kuwapatia abiria
huduma nzuri nyakati za asubuhi na jioni.
Kwenye
safari ya asubuhi, ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 12.00 na
kutua Nairobi saa 1.20. Aidha, safari ya kurudi itaanza saa 1.50 na
itatua Dar es Salaam saa 3.15.
Aidha,
safari mpya za jioni ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 2.15 na
kutua Nairobi saa 3.35. Safari ya kuridi ndege itaondoka Nairobi saa
4.05 na itatua Dar es Salaam saa 5.30.
Kupanuka
kwa ratiba hiyo kutawezesha kusafirisha takribani abiria 19,000 kila
mwezi kupitia safari za fastjet kati ya hiyo miji miwili, na hivyo
kuwapa wasafiri njia nzuri zaidi na mbadala wa safari kwa nauli
wanayoimudu.
“Kila
mara tumekuwa tunaahidi kuongeza masafa yetu ya njia yetu kati ya Dar
es salaam na Nairobi kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka
kunakosababisha na nauli wanayoimudu, usalama, kasi na huduma kwa
wakati,” alisema Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse.
Aliongeza:
“Idadi ya watu jijini Dar es Salaam na Nairobi kwa pamoja ni zaidi ya
milioni themanini ambao wengi wao walishindwa kusafiri kwa ndege
kutokana na ukubwa wa nauli na hivyo tunaamini iliwatenga sehemu kubwa
ywa watu dhidi ya usafiri wa anga lakini hivi sasa wana chaguo la ndege
la uhakika na wanalolimudu.”
Corse
anabainisha kuwa tangu fastjet ianze kufanya safari zake kati ya Dar
es Salaam na Nairobi inakadiriwa kuwa theluthi moja ya abiria wake ni
mara yao ya kwanza kutumia usafiri huo ambao vinginevyo walikuwa
wanashindwa kumudu nauli ya kusafiri kwa njia ya anga kati ya miji hiyo
miwili.
“Kutangazwa
kwa safari 14 za ziada kwa wiki ikiwa ni miezi miwili tu baada ya
fastjet kutangaza kuanza kwa safari za anga kati ya nchi hizi mbili
Januari 11, 2016 kunaonesha msisitizo wa kuongezeka kwa idadi ya wateja
ambao wanaweza kuifikia usafiri wa anga wanaoumudu. Kwa hakikika hili
linaonesha matokeo chanya kwenye maisha ya wananchi na hali kadhalika
kwenye kukua kwa uchumi baina ya nchi hizi mbili,” alisema Corse.
Tiketi
kwa ajili ya safari hizo za ziada kutoka Dar es Salaam tayari ziko
kwenye mauzo ambapo nauli inaanzia shilingi 168,000 za Tanzania kwa
safari moja (bila kodi ya shilingi 102,900) kwa kuondokea Tanzania,
ambapo fastjet inashauri abiria wake kukata tiketi zao mapema kwa ajili
ya siku wanayotaka kusafiri ili kunufaika na nauli zake za chini na
nafuu.
Aidha,
tiketi kwa ajili ya safari hizo za ziada kutoka Nairobi nazo tayari
ziko kwenye mauzo, nauli zinaanzia kwenye dola za Marekani 120 kwa
njia moja (bila kodi ya dola za Marekani 40) kwa kuondokea Kenya, na
vile vile fastjet inawashauri abiria kukata tiketi mapema kabla ya
siku ya kusafiri ili kunufaika na tozo hiyo ya nauli ya chini.
“Safari
za ziada za kurudi jioni inamaanisha kwamba abiria wanaweza kupanga ama
wakutane Dar es Salaam au Nairobi, na kusafiri hadi kwenye maeneo yao
jijini na kurudi nyumbani siku hiyo hiyo,” anasema Corse na kuongeza,
“njia hii na chaguo hili sahihi ni muhimu kwa abiria ambao ni
wafanyabiashara ambao wanakuwa kwenye shinikizo la kubana muda na kuokoa
gharama, na ambao hawataki kulala nje ya maskani yao kwa siku moja au
mbili.”
Matokeo
ya safari za fastjet kwenda na kurudi nchini Kenya tayari ni makubwa ;
ambapo Corse anadokeza kuwa siku ambayo fastjet ilitangaza kuwa
itaanzisha safari za anga kati ya Tanzania na Kenya kwa bei nafuu
ilisababisha mashirika pinzani ya ndege kushusha nauli zao kwa asimilia
40.
“Kimsingi
ukweli unabakia kwamba ushindani ni mzuri kwa wateja. Huwapa chaguo na
husababisha nauli kushuka. Nauli wanayoimudu kunafanya iwe rahisi kwa
wajasiriamali wengi, watalii na wageni wengine kusafiri kati ya
Tanzania na Kenya,” alisema Corse.
Hali
kadhalika kitu kingine kilichopo kwenye njia hizi mbadala ni kuboresha
mizigo inayobebwa na abiria wa fastjet, ikijulikana kama ‘Freighty’
ambayo inamruhusu abiria kusafirisha hadi kilo 80 kwenye mabegi
yaliyokaguliwa kwa shilingi za Tanzania 84,000. Njia hii mbadala
kimsingi imekuwa maarufu miongoni mwa wafanya biashara wanaosafiri na
fastjet kwenye kununua bidhaa za jumla za kimataifa kwa ajili ya
kwenda kuuza kwenye masoko yao ya nyumbani.
Ukataji wa tiketi unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao www.fastjet.com, kupitia wakala wa usafiri aliyethibitishwa na fastjet au kwa kuwasiliana na fastjet kwa njia ya simu +255 784 108 900. Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika kwa fedha taslim, kwa njia ya mtandao au malipo kwa njia ya simu za mkononi.
Mwisho