Mwonekano wa chupa ya bia ya Windhoek inayosambazwa hapa nchini na kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd.
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd Ismail Mzava (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu udhamini wa bonanza lililoandali na Kituo cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge litakalofanyika Viwanja vya Leaders Klabu Jumamosi. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Sas Sangandele.
Mazoezi yakiendelea katika Kituo cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge kilichopo katika Jengo la Tanzanite House lililopo jirani na Kanisa la Full Gaspel.
Mazoezi yakiendelea kwenye kituo hicho.
Vyuma vikiinuliwa kwenye kituo hicho.
Mazoezi yakifanyika.
Hapa ni kazi tu na mazoezi kwa kwenda mbele.
Na Dotto Mwaibale
KITUO cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge kimeandaa bonanza la michezo mbalimbali litakalofanyika Jumamosi Viwanja vya Leaders Klabu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Sas Sangandele alisema bonanza hilo liwatawahusisha watu wa rika zote wakiwepo watoto.
"Bonaza letu litawashirikisha watu wa aina zote na litakuwa la bure na litaanza saa 12 asubuhi hadi jioni hivyo wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongaji vyake tunawaomba wafike kwa wingi kushiriki" alisema Sangandele.
Alisema bonanza hilo ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd kupitia kinywaji chake cha Windhoek linakuwa na michezo ya mpira wa miguu, kufukuza kuku, karate kwa watoto, mazoezi ya viungo na mbio za kilometa tano.
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo, Ismail Mzava alisema wameamua kudhamini bonanza hilo kutokana na umuhimu wa michezo ambayo inaleta afya kwa jamii.
"Kampuni yetu imekuwa ikitoa udhamini mbalimbali katika shughuli za jamii ndio maana tukaona ni vema tukawaunga mkono hawa wenzetu katika jambo hilo muhimu litakalohusisha michezo mbalimbali" alisema Mzava.