MIAMBA YATEMBELEA MWAMBA WA NGORONGORO.*
Ikiwa ni majira ya Masika na kiubaridi, Bustani ya Eden ya Ngorongoro ikizungukwa na kingo zenye urefu wa Mita 610 huku wanyama na ndege wakichagiza kwa sauti murua zinazoashiria kuwa Ngorongoro ni mwamba wa miamba usiotikisika na kusheheni msingi imara wa vivutio vya asili, urithi wa utamanuni na maajabu saba katika eneo moja.
Miamba inayounda Bodi ya Wakurugenzi ikiongozwa na makamu mwenyekiti Dkt Harrieth Mtae inatembelea hifadhi ya Ngorongoro kuanzia ofisi za makao makuu hadi Kreta ya Ngorongoro na kujionea Eden hiyo ikiwa imesheheni kila aina ya ufahari unaoweza kuelezeka kidunia.
Bodi hii ni sawa na miamba ndani ya Mwamba kwani imejaa wabobezi katika masuala mengi ikiwemo ulinzi,uhifadhi, uchumi, ikolojia, maendeleo ya jamii, ukaguzi, sheria, utawala na diplomasia
Kubwa wanalilosisitiza kwa menejimenti “mnafanya kazi nzuri endeleeni kuchapa kazi na tangazeni kitaifa na kimataifa fahari ya Ngorongoro ambayo ni kivutio bora cha Utalii Afrika mwaka 2025

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia