DKT. TOBA NGUVILA AWASILI ARUSHA NA KUSISITIZA KIPAUMBELE KATIKA SEKTA YA UTALII🇹🇿





Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Alnason Nguvila amewasili mkoania Arusha, tayari kwa kuanza rasmi kazi ya kutumikia wadhifa huo na kupokelewa na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha ikiongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Mkoa, Ndugu Mosses Pesha


Akiwa ofisini hapo, Dkt.Nguvila amesaini kitabu cha wageni na kupata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya watumishi wa Umma wa Mkoa huo, wakiwemo Sekretarieti ya mkoa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma Mkoa wa Arusha, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Tarafa, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa mkoa huo.


Hata hivyo Katibu Tawala huyo, ametumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kukutana na wanaArusha, amemshukuru Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kumuamini na kumteua  kushika nafasi hiyo katika Mkoa wa Arusha.











About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia