MWENGE WA UHURU WAZINDUA UJENZI WA TENKI LA MAJI KIMINDOROSI




Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda amezindua mradi wa ujenzi wa Tenki la maji Kimindorosi lenye ujazo wa Lita elfu 50 Kata ya Olasit, mradi uliotelekelezwa na Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha - AUWSA mapema leo Julai 09,2026.


Akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi Rasilimali watu, Kazimili Reuben Kanyanza amesema kuwa, mradi huo umetekelezwa na mafundi wa Mamlaka hiyo ya maji AUWSA kwa gharama ya shilingi milioni 93, shilingi milioni 2.5 ikiwa ni michango ya wananchi na shilingi Milioni 93.3 fedha kutoka Serikali Kuu.


Akizindua mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda ameishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi ya maji nchini, na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya Kumtua mama ndo kwa kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi kwenye maeneo yao.


Mwang'onda amethibitisha namna Serikali ya awamu ya sita inavyotekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa kutoa fedha nyingi za kutekelza miradi ya maji nchini huku Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akidhamiria kumtua mama ndoo kichwani kama ilivyo kwa wakazi wa Kimondosi.



"Tunamshukuru Mhe Rais kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji karibu na maeneo yao, leo Kina mama wa Kimondorosi wanakiri kuondokana na adha ya kwenda kutafuta maji mbali.


Awali Katika wilaya ya Arusha Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Km 89.2 na utatembelea jumla ya miradi 7 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9.


Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026 'Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuijenga'











About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia