HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI YAPONGEZWA KWA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.
Wazo Mwang'onda Mkimbiza Mwenge Kitaifa aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza suala la matumizi ya Nishati Safi kwa Taasisi za Umma na Binafsi zilizomo Wilayani humo.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ⅞ ya Nishati Safi ya kupikia Mwl. Godfrey W. Mngoma Mkuu wa Shule ya Sekondari Alpha Omega amesema kuwa Shule hiyo inatekeleza mradi wa matumizi ya Nishati safi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani za kulinda Mazingira, kuboresha Afya za Wananchi na kupunguza matumizi ya Kuni na mkaa katika Taasisi Binafsi na za Serikali.
Aidha, katika kutekeleza juhudi hizo Halmashauri imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia ambapo shule hiyo ya Alpha Omega imetekeleza kwa kukamilisha mradi wa matumizi ya Nishati safi wenye jumla ya shilingi Milioni 20 kwa kuweka gesi, kufunga na kununua majiko matano yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya Wanafunzi 500 na gharama za uendeshaji kwa kila miezi mitatu ni shilingi Milioni 2.8
Vile vile, ameeleza kuwa jumla ya vikundi 80 vya Baba na Mama Lishe vimegawiwa mitungi ya gesi sambamba na Halmashauri hiyo kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa Maasai Stoves na ENCHO ili kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa wananchi.
Gloriana Kimath Mkuu wa Wilaya ya Monduli amesema kuwa, Wilaya ya hiyo inashirikiana vyema na Wadau mbalimbali katika kutekeleza suala la matumizi ya Nishati Safi na kupelekea Wananchi kuondokana na matumizi ya Kuni na makaa yanayopelekea kuharibu mazingira.
NWazo Mwang'onda amehitimisha kw kusema kuwa mtungi mkubwa, majiko matano pamoja na mitungi midogo ambayo ipo tayari kutumika endapo mtungi mkubwa ukiishiwa, ni hatua kubwa ya kuunga mkono Juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Mazingira yanatunzwa na Afya za Wananchi zinaimarika sambamba na kuwapongeza Mama lishe kwa kutumia Nishati safi ya kupikia.
![]() |




0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia