WAZAZI WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO MALEZI NA ULINZI WA MTOTO

 Wazazi wametakiwa kutimiza wajibu wao katika malezi na ulinzi wa mtoto ili kuhakikisha watoto wanakua katika mazingira salama yasiyo na vitendo vya ukatili.


Wito huo umetolewa na Mkaguzi Msaidizi Emmanuel Kisiri, ambaye ni Polisi wa Kata ya Ikoma, alipokuwa akitoa elimu ya Polisi Jamii katika nyumba ya Abwire Thomas hivi karibuni.

Mkaguzi Msaidizi Kisiri amesema wazazi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwalea, kuwafuatilia na kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zinazoweza kuhatarisha ustawi wao.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya wazazi, jamii na vyombo vya ulinzi na usalama ni muhimu katika kujenga mazingira bora ya malezi na kuhakikisha haki za watoto zinazingatiwa.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia