WAWILI WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA ATHARI ZA MVUA MIROGORO
![]() |
| Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama |
Na Lilian Kasenene,
WATU wawili wamefariki Dunia na wengine wawili kujeruhiwa kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro huku wananchi wakitakiwa kuchukua tahadhali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama alithibitisha kutokea kwa vifo na majeruhi, na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Mkama alisema tukio hilo limetokea Februari 23,2026 Majira ya usiku huko katika kitongoji cha Mbesi, Kijiji na Kata ya Utengule Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Tano Leonard Lunasi(36) na Ngimila Ndombeji Mashana(27) wote ni wakulima, wakazi wa kitongoji cha Mbesi.
Waliojeruhiwa ni Manyanda Ramadhani Masasila(35) na Michael Aloyce Msanga(28) wote wakulima, wakazi wa kitongoji cha Mbesi.
"Hawa marehemu na majeruhi walipigwa na radi wakiwa njiani wakati wakitoka matembezini,"alisema kamanda huyo wa Polisi Morogoro.
Majeruhi Michael na Manyanda walitibiwa na kuruhusiwa.
Kamanda wa Polisi Mkama amewaomba wananchi mkoani hapa kuendelea kuchukua tahadhali wakati wa kipindi hiki cha mvua zinapoendelea kunyesha ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo ya vifo.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia