SERIKALI YASISITIZA MAGEUZI YA KILIMO KUPITIA SHOROBA ZA KILIMO
Na Woinde Shizza, Arusha
Serikali imesema mageuzi ya sekta ya kilimo kupitia shoroba za kilimo ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa mpango wa taifa wa kukuza uchumi, kuongeza ajira na thamani ya mazao nchini ,hatua hiyo inalenga kufanya kilimo kuwa injini kuu ya maendeleo ya viwanda na
Aidha serikali imejipanga kubadilisha mfumo wa kilimo wa mazoea na kuelekeza nguvu katika kilimo cha kibiashara chenye tija kwa wananchi na kubainisha kilimo kinachangia asilimia 26.5 ya pato la taifa na zaidi ya asilimia 30 ya ajira nchini.
hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Tanga Batilda Buriani amebainisha hayo leo Jijini Arusha wakati akifungua Kikao kazi cha uhamasishaji na uendelezaji wa Shoroba za Kilimo ili kujenga uelewa wa pamoja miongoni mwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya, wataalamu wa Mikoa na Halmashauri, kuhusu shoroba za kilimo na nafasi yake katika ukuzaji wa kilimo, ikiwa ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa mpango kabambe wa uendelezaji wa mageuzi ya kilimo nchini.
Aidha Batilda akieleza namna ambavyo kilimo kimekuwa muhimu kama sekta ya kimageuzi nchini, amerejea maandalizi ya Mkoa wa Arusha kuelekea michuano ya AFCON 2027, akisema mahitaji ya chakula yatakuwa makubwa na hivyo ni muhimu wananchi wakaandaliwa kuchangamkia fursa hiyo ya chakula wakati wa michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa Mpira wa miguu kwa Timu za Taifa
"Leo Mkoa wa Arusha upo kwenye mkutano wa maandalizi ya AFCON, utashangaa viazi wakati wa AFCON 2027 vitatoka Njombe au mpunga utoke Mwanza, Shinyanga au Tabora ilihali hapa tuna mabonde ya kutosha. Hapa hatujaja kwa bahati mbayaz tumekutana tuone namna ambavyo kila mdau atatumia fursa zilizopo kuimarisha kilimo, mapato, uchumi, ajira kwa Vijana na zaidi kuongeza thamani na kulinda mazingira." Amesema Mhe. Burian.
Alisema serikali imesisitiza kulindwa kwa maeneo ya kilimo dhidi ya matumizi yasiyo sahihi na kurejesha kilimo cha kahawa kutokana na ongezeko la mahitaji ya zao hilo duniani ,Pia amehimiza matumizi ya
teknolojia za kisasa, ikiwemo Smart Agriculture, na kuwawezesha vijana kupata elimu na masoko ya uhakika.
Aidha alihitimisha kwa kusema kuwa mageuzi ya sekta ya kilimo hayawezi kufanikiwa bila ushirikiano wa wadau wote “Wakulima ndio uti wa mgongo wa taifa letu, hivyo kila mmoja lazima awajibike kuhakikisha kilimo kinakuwa chanzo kikuu cha ajira na uchumi wa taifa,” alisema.
Kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wa wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi, kimefadhiliwa na Serikali ya Norway kwa lengo la kuwajengea viongozi uelewa wa pamoja kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.
Mkurugenzi wa SAGCOT, Godfrey Kirenga, alisema shoroba za kilimo ni maeneo ya kimkakati yanayounganisha ardhi, biashara na mazingira kwa lengo la kuharakisha maendeleo chanya kwa wakulima na kuvutia wawekezaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (ATO), Dkt. Elizabeth Missokia, alisema ofisi hiyo ilianzishwa mwaka 2013 kusimamia mageuzi ya kilimo yanayowiana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ikiwemo matumizi ya mfumo wa AgriCore unaolenga kuongeza tija na thamani ya mazao.
Serikali pia imepanga kutumia Bandari ya Tanga kama kituo maalum cha kusafirisha bidhaa za kilimo nje ya nchi ili kuongeza mapato, kukuza biashara na kuimarisha mnyororo wa thamani wa mazao ya wakulima wadogo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, alisema maeneo ya kanda ya kaskazini yanaendelea kutumia teknolojia na mbinu za kisasa zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi, jambo linaloongeza uzalishaji na ubora wa mazao.






0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia