MADIWANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO YA ASILIMIA 10
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mheshimiwa Maximilian Iranghe amewataka Madiwani wa Kata za jiji la Arusha kuhakisha wanawajengea mazingira mazuri makundi maalumu kupata mikopo ya asilimia 10 itolewayo na halimashauri hii.
Ametoa Rai hiyo hii leo wakati wa ufunguzi wa Kikoo Cha pili Cha Baraza la madiwa Robo ya pili ambapo KIKAO hicho Cha Robo ya pili kilihudhuriwa na mkuu wa wilaya Joseph Mkude pamoja na wageni mbalimbali.
Amesema kuwa haileti picha nzuri kwa Diwani katika Kata aliyochaguliwa kukiwa vikundi maalumu wakiwemo Wakina mama, Vijana na Walemavu kukosa kutokana na kukosa vigezo vya kuweza kupata mikopo na kuwataka kuwatengenezea mazingira ya kuweza kupata mikopo hiyo itokayo halimashauri.
" Ni kitu cha kusikitisha kwa Diwani mwananchi wako anakosa mkopo kwa kigezo Cha kutokuwa na makazi ya biashara, wapelekeni katika Masoko tuliyo yaandaa ili wapate kigezo cha kukopesheka na halimashauri", Alisisitiza mstahiki MEYA.
Pamoja na hayo mstahiki Meya wa jiji la amewataka watumishi wa jiji la Arusha kuhakisha wanadai takribani Bilioni 3 za mikopo hiyo ya nyuma ambao walikopa hawajarudisha ili kuwezesha kupanua wigo wa mikopo hiyo ya asilimia 10 ya mapato ya halimashauri.




0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia