NABII MKUU PROF. GEORDAVIE ATUNUKIWA CHEO CHA UPROFESSOR
WAZIRI KABUDI AANGAZA UHUSIANO KATI YA ELIMU, AMANI NA USHIRIKIANO
Na Woinde Shizza, Arusha
Katika hafla ya kihistoria iliyofanyika katika Nyumba ya Matamko Ngurumo ya Upako Kisongo, Arusha, dunia ya elimu na dini ilishuhudia tukio la kipekee ,ambapo Nabii Mkuu Prof. Geordavie ambae pia ni balozi wa amani alipewa cheo cha Uprofessor wa Kitaaluma, tukio lililothibitisha uthubutu wake wa kielimu na mchango wa kiroho.
Mgeni rasmi wa tukio hilo , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu Ikulu, Prof. Palamagamba Kabudi, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani, alibainisha kuwa cheo hiki sio heshima tu, bali ni uthibitisho wa ujuzi, maarifa na mchango wa kiakademia.
Elimu: Msingi wa uongozi bora
Prof. Kabudi alisisitiza kuwa viongozi wa kanisa na jamii wanapaswa kuendeleza elimu yao ili kuelewa masuala ya kidini na kijamii kwa kina.
“Elimu ni msingi wa uongozi bora na heshima katika jamii,”
alisema Kabudi, akiongeza kuwa uelewa wa kina husaidia kiongozi kushughulikia changamoto za kisasa, kuwa mfano wa kuigwa, na kuhamasisha vijana.
Faida za elimu ya juu kwa viongozi wa dini
Prof. Kabudi alibainisha kuwa elimu ya juu inatoa Uelewa wa kina wa neno la Mungu,
Uwezo wa kukabiliana na teknolojia na sayansi za kisasa,
Kudumisha amani na mshikamano wa kijamii,
Ushirikiano na wataalamu kutoka nyanja mbalimbali
“Viongozi waliyoelimika wana uwezo wa kushirikiana bila kupoteza misingi ya imani na maadili,”
alisema Kabudi, akisisitiza mchango wake katika jamii yenye mshikamano, umoja, na maendeleo endelevu.
Mafanikio ya Prof. Geordavie
Prof. Kabudi pia alionyesha mafanikio ya Prof. Geordavie, na kubanisha kuwa amesoma vitabu vyake alivyo vizindua ambapo vinaelezea diplomasia ya kimataifa na ushirikiano wa kimkakati wa Afrika vikiwa ni mwanga kwa uongozi wa amani.
Kwa upande wake, Prof. Geordavie alikumbuka tuzo yake ya kimataifa ya Amani (International Law Mayor of Peace Award) iliyotolewa na International Association of World Peace Advocates kwa kushirikiana na Association of the United Nations, jijini Nairobi, Kenya, tarehe 7 Januari 2025.
Alieleza dhamira yake ya kuunda jamii yenye maadili, mshikamano, na inayoheshimu misingi ya amani na haki, huku akisisitiza nafasi kubwa ya Afrika katika ushirikiano wa kimataifa.
Aidha hafla hiyo imeonyesha wazi jinsi elimu, uongozi wenye maadili, na ushirikiano wa kimataifa unavyoweza kuchangia maendeleo, mshikamano, na amani katika jamii.
Tukio hili limeweka mfano wa viongozi wanaoweza kuunganisha maarifa na maadili ili kuendeleza ustawi wa jamii.
Kwa ujumla, tukio hili limebainisha wazi kuwa elimu, uongozi wenye maadili, na mshikamano wa kimataifa ni silaha za msingi ya kuendeleza jamii yenye amani, mshikamano, na maendeleo endelevu.








0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia