MAHAKAMA YAAHIDI UADILIFU KATIKA UTOAJI HAKI

 MAHAKAMA YAAHIDI UADILIFU KATIKA UTOAJI HAKI

Yawataka wadau wote kushirikiana na kutenda haki



Na Woinde Shizza, Arusha


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Frank Mahimbali, amesisitiza umuhimu wa Mahakama kuwa kimbilio la wanyonge na ngao ya haki, akisema ni nguzo muhimu katika utawala wa sheria, haki na uwajibikaji kwa maendeleo ya Taifa.


Akizungumza leo, Jumatatu Februari 2, 2026, wakati wa kilele cha Siku ya Sheria nchini kilichofanyika katika Viwanja vya Mahakama Kuu jijini Arusha, Jaji Mahimbali amewataka Majaji, Mahakimu na Mawakili kutambua unyeti wa nafasi zao katika maendeleo ya nchi kwa kusikiliza na kutoa maamuzi kwa haraka, akibainisha kuwa Mahakama ya Tanzania ni chombo cha haki, demokrasia na utawala bora.


Katika hatua nyingine, Jaji Mahimbali amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  CPA Amos Gabriel Makalla, kwa ukomavu na ushirikiano wake na Mahakama, akisema anathamini mchango wa chombo hicho katika kulinda haki za wananchi.


Ameapa kuwa hatovumilia dharau wala kejeli kwa Mahakama, akisisitiza kuwa ni lazima chombo hicho kiendelee kuwa cha kuaminika, chenye uadilifu na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.





Awali, katika salamu zake za ukaribisho,  Makalla aliahidi kuendelea kushirikiana na Mahakama katika kutatua migogoro kwa njia mbadala na kuhakikisha utekelezaji wa hukumu zinazotolewa unafanyika ipasavyo.


Ametoa wito kwa Mawakili na Watumishi wa Mahakama kuzingatia uadilifu katika kuwahudumia wananchi na kutoa elimu ya sheria ili kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao.




About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia