RC ARUSHA AWATANGAZIA MACHINGA, BODABODA, MAMALISHE, WAJASIRIAMALI NA WASAFIRISHAJI FURSA ZA BUNGE LA IPU*
. *_Awataka wachangamkie fursa za biashara_*
. *_Awahimiza kuzingatia usafi, usalama na ukarimu katika utoaji wa huduma_*
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumanne Septemba 22, 2026 amekutana na Makundi ya Machinga, Bodaboda, Mama na Babalishe, Wajasiriamali na Madereva wa Bajaji na kuwataka kuchangamkia fursa za Ujio wa Mkutano wa Bunge la 153 la dunia (IPU), unaotarajiwa kufanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia Oktoba 05, 2026.
Katika maelezo yake, kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, Mhe. Makalla ameitaja Tanzania kama Nchi ya amani, Arusha kama Mkoa wa Utalii na wenye watu wakarimu na kuyataka Makundi hayo kuwa mabalozi wa vitu hivyo katika kipindi chote cha Bunge la IPU, wakati wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji na Biashara la Horticulture (HortiLogistica Africa 2026) pamoja na kwenye michuano ya soka kwa Timu za Taifa za Afrika, AFCON 2027.






0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia