ARUSHA KUWA KITOVU CHA MIKUTANO YA KIMATAIFA
Amshukuru Mhe. Rais Samia kwa uwekezaji wake katika ujenzi wa Ukumbi wa Kimataifa, Mkubwa zaidi Afrika
Ukumbi wa AICC waendelea kupokea Mikutano ya ndani na Kimataifa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amesema Mkoa wa Arusha unaendelea kuwa kitovu cha mikutano ya kimataifa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu mbalimbali yenye kuifanya Arusha kuwa chaguo la Mikutano hiyo.
Makalla ameyasema hayo leo Alhamisi, Septemba 17, 2026, katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), akimshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watu 5,000 kwa wakati mmoja kwenye Ukumbi mkuu na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na ukumbi mkubwa zaidi barani Afrika.
Mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Makalla amesema uwekezaji huo unaenda sambamba na ujenzi wa hoteli ya kifahari itakayokuwa na vyumba 500 pamoja na kumbi nyingine ndogo zitakazoweza kuhudumia washiriki kati ya watu 30 hadi 500.
Aidha amesema AICC imeendelea kupokea na kuwa mwenyeji wa mikutano mbalimbali ya ndani na kimataifa ikiwemo Mkutano wa Bunge la Dunia IPU, Mwezi Oktoba mwaka huu, hali inayoendelea kuifanya Arusha kuwa eneo muhimu la mikutano na matukio makubwa ya Kitaifa na Kimataifa, akiahidi kuimarisha usalama, mazingira wezeshi ya mikutano na ushirikiano na wadau ili kufanikisha Mikutano hiyo.



0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia