kamanda Sabas akionyesha silaha ,risasi na mihuri ambayo majambazi hao wamekuta nazo
kanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari vifaa vilivyokuwa vinatumika kuoshea silaha aina ya smg ambazo wamekutwa nazo majambazi hayo
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu watatu wakiwa na silaha aina ya pisto yenye risasi tano pamoja na mashine ya kuonyesha bunduki , kifaa cha kubustia risasi pamoja na risasi 46 za bunduki aina ya smg Katika matukio mawili tofauti.
Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa matukio hayo mawili yalitokea kwa nyakati tofauti Katika maeneo tofauti ya mkoani hapa kufuatia msako mkali uliokuwa ukifanya na jeshi la polisi pamoja na ushirikiano wa wananchi wasamaria wema.
Alisema kuwa Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Salimu Kiwele alimaarufu kwa jina la Msaula(39)mkazi wa sombetini mkoani hapa akiwa na mke wake aliyetambulika kwa jina la Princes Juma (34) wote ni wakazi wa sombetini wamekamatwa nyumbani kwao wakiwa na silaha pamoja na risasi.
Alisema kuwa watu hao walikamatwa wakiwa na silaha aina ya pisto Glock FFN 350 ikiwa na risasi tano ambazo zilikuwa ndani ya magazine ya silaha hiyo.
Alisema kuwa mtu huyu pamoja na mke wake walikuwa wanatafutwa na polisi kwa kipindi cha mda mrefu kufuatia kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ,mauaji pamoja na wizi ambao yameshawai kutokea jijini hapa .
Katika tukio lingine kamanda sabas alisema kuwa mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Konsolata Tarimo (30)mkazi wa ngaramtoni amekamatwa na jeshi la polisi akiwa na risasi 46 za bunduki aina ya smg pamoja na vifaa mbalimbali za bunduki hiyo ikiwemo kifaa cha kusafishia silaha hiyo.
Alibainisha kuwa mwanamke huyo alikutwa nyumbani kwake majira ya saa nane usiku wa kuamkia September 6 wakati askari waliokuwa doria walipofanya msako wa kushutukiza Katika nyumba hiyo mara baada ya kutilia shaka.
Walisema kuwa walipofanya msako huo walikuta risasi hizo 46 za bunduki hiyo aina ya smg ,muhuri ambao ulikuwa umeandikwa pande zote mbili huku pande ya kwanza ikiwa imeandikwa District game office simanjiro na upande mungine umeandikwa district game of monduli district,kifaa cha kubusti risasi Katika bunduki hiyo ya smg pamoja na kifaa cha kusafishia silaha hiyo inayotumiwa na risasi hizo.
Aidha alibainisha kuwa silaha ambayo ilikuwa inatumika kwa ajili ya silaha hiyo haijakamatwa bali msako mkali unaendelea ili kukamata silaha hiyo iliyokuwa ikitumia risasi hizo.
Alisema kuwa watuhumiwa wote bado wapo chini ya ulinzi kwa ajili yamahojiano na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani araka iwezekanavyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia