Naibu Waziri wa Afya, Dk Seif Seleman Rashidi amesema tatizo la
unywaji wa pombe wakati wa kazi ni kubwa na linaathiri jamii kama
kuvunjia kwa ndoa, ajali za magari barabarani, magonjwa na kurudisha
nyuma maendeleo ya mtu binafsi au nchi.
Kutokana na madhara hayo, alisema serikali ipo kwenye mchakato wa
kutunga sera itakayosaidia kudhibiti unywaji wa pombe wakati wa kazi.
Alisema iwapo serikali itafanikiwa kuwa na sera ya kudhibiti matumizi
ya pombe, itasaidia kuongeza uchumi wa nchi kwani unywaji pombe
unapunguza nguvu kubwa ya taifa.
Alisema kwa mfano, kwa sasa tatizo la unywaji wa pombe limekuwa
linawafanya vijana wengi kushindwa kufanya kazi pamoja na
kuzitawanyisha familia nyingi hali ambayo inasababisha ongezeko kubwa
la watoto wa mitaani.
“Nadhani iwapo sera ya nchi ya udhibiti wa unywaji wa pombe ikiwepo
madhara haya yote hayatakuwepo hata na nchi yetu itaondokana na
matatizo mbalimbali yakiwemo ya watoto wa mitaani, ongezeko la
maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, uvunjifu wa ndoa nyingi ambazo
zinapelekea ongezeko la watoto wa mitaani,” alisema.
Aidha alibainisha kuwa watu wanaokunywa pombe kupita kiasi mara nyingi
huwa hawapati lishe bora na hivyo kuongoza kasi ya vichocheo vya
magonjwa kwa mfano mtu aliyeathirika na Virusi Vya Ukimwi (VVU) iwapo
atakuwa anatumia pombe basi atajihatarishia maisha yake kwani
anapunguza CD4 na pia huchangia kupoteza hamu ya kula kabisa.
Alisema kauli mbiu ya mkutano huu ni pombe inaleta matatizo katika
jamii hivyo suala hilo lishulikiwe sasa kwani pombe sio kitu cha
kawaida na sio chakula hivyo wananchi wanapaswa kujua hilo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari
Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema wao kama chama cha waandishi
wa habari wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa wanawake
ambao wamefanyiwa vitendo vya ukatili ambao mengi yao yanasabishwa na
unywaji wa pombe kupita kiasi.
Mbali na hilo alibainisha kuwa kitu kingine kinachopeleka unyanywaji
wa pombe kupita kiasini ni matangazo ambayo yanarushwa na
yanahamasisha unywaji wa pombe kwani matangazo hayo yamekuwa
yanahamasisha vijana na watu wa rika mbalimbali kunywa pombe kwani
yanaelekeza kuwa hata wenzetu wanchi za nje wanatumia vilevi hivyo.
Aidha nkya aliitaka serekali kutenga fedha za kufanya tafiti
zakutosha na kudhibiti unywaji mbaya wa pombe ili wananchi waweze
kusikia na kuacha maswala hayo .
Mkutano huu wa umuhimu wa kuwa na sera ya matumizi vileo katika nchi
za Malawi, Sweden na Jumuiya ya Afrika Mashariki umeshirikisha wadau
mbalimbali wakiwemo wabunge wa nchi wanachama pamoja na wataalam wa
kimataifa wa mambo ya vileo na mambo ya jamii nchi za jumuiya.