BREAKING NEWS

Monday, September 10, 2012

WANAWAKE WA TANZANIA WAPETA SAFARI MARATHONI NAALI AMWAGWA ASHIKA NAFASI YA TATU


  meneja mauzo wa bonite Gilberty Oiso
  mkuu wa wilaya ya arusha mjini John Mongela akiwa anakimbia mbio za kilometa 21 lakini akufanikiwa kumaliza kilometa zote ambapo aliahidi mwakani atakipia zote





 Timu nzima ya serena  hotel


 Watoto wa timu ya chaki walishiriki na kushika nafasi za mwanzo
 meneja mauzo wa bonite Gilberty Oiso akiwa anampita mpinzani wake dr.Makani katika mbio za safari marathoni ,meneja huyu alikimbia kilometa 21 na akamaliza bila matatizo

MISOSI usipime ni balaa mishikaki iliyekuwepo kwenye safari marathon


ikionyesha washindi wanawake tatu bora wa kwanza akiwa ni Jackline sakiru  katika kati wapili ni Agnrss katungi kutoka kenya na Mary naali kutoka tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao

 ikionyesha washindi wanawake tatu bora wa kwanza akiwa ni Jackline sakiru  katika kati wapili ni Agnrss katungi kutoka kenya na Mary naali kutoka tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao

Imebainika kuwa washiriki wengi wa mchezo wa riadha hapa nchini wamekuwa wakishidwa kufikia malengo yao kutoka na kushindwa kufanya mazoezi jinsi inavyotakiwa.

Hayo yamebainishwa na mshindi wa kwanza wa mashndano yasafari marathoni Jacline sakiru wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mbiozake za kilometa 21  na kuwa mshindi zilizofanyika jijini hapa.

Alisema kuwa wanariadha wengi hapa nchini wamekuwa hawaati muda wa kutosha wa kufanya mazoezi hali ambayo inasababisha kutofanya vyema katika mashindano mbalimbali ambayo wanashiriki

"tukichukulia mfano mashindano ya olimpiki ambayo yamemalizika hivi karibuni watanzania tumeshindwa fanya vyema kutokana na uzembe wetu wewe kweli timu ya taifa inayoiwakilisha taifa itakaa kambini miezi miwili na kwenda kwenye mashindano hauoni huo ni wizi mchezaji atajiandaaje katika kipindi hicho ukiangalia mchezaji huyo anaenda kushindana na nchi kama kenya na ethiopia kweli tunatakiwa kuwa  makini sana katika riadha yetu tusipo angalia tutabakia kushika mkia"alisema Sakiru

Aidha katika mashindano hayo ya safari marathoni wanawake waliweza kufanya vyema katika mbio za kilometa 21 kwani katika nafasi ya kwanza mwanamke ambaye ni mtanzania Jackiline sakiru aliweza kushika nafasi ya kwanza ambapo alitumia muda wa 1:13:22 ,huku  nafasi ya pili ikishikiliwa na mkenya Agness Katungi ambaye alitumia muda wa 1:14:12 na watatu akiwa ni mary naali kutoka tanzania ambaye alitumia muda wa 1:15:13  huku nafasi ya nne ikishikwa na mtanzania Christine Muyanga kutoka kenya ambaye alitumia muda wa 1:16:47 na Catherin Range kutoka Tanzania ndie aliyeshika nafasi ya tano ambaye alitumia muda wa 1:17:24 .

Kwa upande wa wanaume kilometa 21 charls orgar aliweza mkenya aliweza kufanya vyema na kushika nafasi ya kwanza ambapo alitumia muda wa 1:04:48,nafasi yapili ikishikwa  na mkenya tena Elija Mtuei ambaye alitumia muda wa 1:04:57 huku  watanzania Paschal mombo akishika nafasi ya tatu ambaye alitumia muda wa 1:04:59 na watano akitumia muda wa 1:05:15 ambaye alitambulika kwa jina la Daniel Mandi mchezaji ambaye mwaka juzi alishikilia nafasi ya kwanza katika mashindano haya.

Gazeti hili lilizungumza na mmoja wa wathamini wa mbio hizi za safari marathon ambaye ni meneja masoko wa Tourism Promotion serveces  (TPS) ambao wamethamini mashindano haya kupitia hotel ya ya serena  David Sem naye alisema kuwa anawapongeza sana waandaaji wa mashindano haya kwani wameweza kufanya vyema katika mashindano haya kwani wameaandaa kitu kizuri ambacho kinaweza kukuwakusanyisha watu wakubwa kwa watoto ili waweze kukaa pamoja na kubadilishana awazo pamoja na ku saidia kuweka viungo vyema.

Alisema kuwa mashindano haya yanawasaidia wao kama wafanya biashara kujitangaza pamoja na kuwasiadia kukutana na watu mbalimbali kutoka katika nchi mbalimbali na kubadilishana mawazo ya kibiashara pamoja na ya kijamii.

Aliwasihi wananchi kujitokeza kushiriki mashindano haya kwani yanasaidia mambo mengi huku akiwasihi viongozi mbalimbali ,makampuni pamoja na taasisi kujitokeza kuwekeka katika mchezo huu wa riadha kwani chezo huu ni kama michezo mingine ile  na iwapo watasaidia kuthamini wachezaji mbalimbali pia watakuwa wamepaa fursa yakujitangaza pamoja na kuitangaza nchi yetu vyema.

kwa upande wake meneja mauzo  wa kampuni ya Bonite Gilnerty Oiso  alisema kuwa kampuni hii kupitia kinywaji chake cha coca cola wamejitolea kuthamini mashindan haya kila mwaka kwani mashindano haya yanasaidia kuinua vipaji vya riadha kwa watoto na vijana hapa nchini.

Alisema kuwa wao kama bonite ni mara yao ya tatukushiriki mashindano haya na wanafurahia kwani wanaona waandaaji wa mashindano haya wanayaboresha siku hadi siku.

Aidha alitoa wito kwa wananchi kwa ujumla kushiriki katika mchezo huu haswa katika mashindano haya ya safari marathon ambayo kwa mwaka yanafanyika mara moja na mbali na hapo aliwasihi wananchi kushiriki katika michezo mbali mbali kwani wakishiriki hawataweza kupata magonjwa nyemelezi yanayowakumba watu mara kwa mara.

Naye mratibu wa mashindano haya victor mollel alisema kuwa mashindano yanaenda vyema kwani wamemaliza salama huku akibainisha kuwa watu wanazidi kuongezeka kila mwaka huku akibainuisha kuwa katika mwaka uliopita watu 700 walishiriki na kwamwaka huu watu zaidi ya 1500 wameshiriki mashindano haya huku akitoa wito kwa wanachi kuendelea kushiriki kila mwaka .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates