BREAKING NEWS

Friday, September 14, 2012

Flag this message DKT. BILAL AZINDUA MKUTANO WA 14 WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA BARANI AFRIKA JIJINI ARUSHA

 Meneja Mkuu wa Uwezeshaji wa Shirika la Manedeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Ishmael Dodoo akimwongoza Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (wa tatu kulia) alipowasili katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano (AICC) kuhuduria mkutano wa 14 wa Mazingira na Uzinduzi wa mtandao wa Mazingira unaosimamiwa na NEMC.
 Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kulia) akisikiliza Wafanyakazi wa UN Harriet Macha na Katibu wa klabu za Umoja wa Mataifa mkoa wa Kilimanjaro Angaja Fundisha wakitoa maelezo kwa wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Arusha.

Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa hapa nchini Dr. Alberic Kacou wakishikana mkono na kusalimiana na Dr. Mohamed Abdel-Monem wakati wakisubiri kuingia katika ukumbi wa mkutano wa Mbayuwayu uliopo AICC.
Bw. Ishmael Dodoo wa UNDP wakijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal (Kulia) akiwa meza kuu na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoros Dr. Fouad Mohdji (katikati) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wa Mazingira wa Tanzania.

Waziri Afisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akitoa ripoti juu ya mtandao wa Mazingira utakavyokuwa ukifanya kazi, akifafanua juu ya mtandao huo na moja ya kazi zake kuwa ni kufikisha kwa wananchi habari za mazingira juu ya uharibifu na utengenezaji wa mazingira hapa nchini.
Waziri Afisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akitoa ripoti juu ya mtandao wa Mazingira utakavyokuwa ukifanya kazi, akifafanua juu ya mtandao huo na moja ya kazi zake kuwa ni kufikisha kwa wananchi habari za mazingira juu ya uharibifu na utengenezaji wa mazingira hapa nchini

Wanafunzi wa sekondari ya Ilboru wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwenye banda la maonyesho wakati wa mkutano wa 14 wa Mazingira jijini Arusha. Kulia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa UN Sangita Khadka Bista, Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha UN (UNIC) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu.


Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dr. Alberic Kacou akielezea amesema huu mkutano wao kama Umoja wa Mataifa ni kuweka misingi na uwezeshaji ambayo inayoletwa na Serikali za mataifa mbalimbali ambao ni wanachama wa Umoja huo juu ya Suala zima la maendeleo na mazingira na changamoto zinazoyakibili mazingira  na kusaidia Utawala juu ya swala zima la ardhi ikiwemo misitu kwa ujumla na kuwawezesha fedha juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mazingira kwa ujumla juu ya utumiaji na utunzaji wa mazingira halisia.
 adhi ya Wataalamu wa Mazingira wakimsikiliza Makamu wa Rais (hayupo pichani) wakati akifafanua jambo juu suala zima la mazingira na udhibiti ili tuendele kuwa mfano na kuapa zawadi nyingine juu ya utunzaji wa mazingira na gesi ya ukaa ya Ozoni hapa nchini kwetu.



Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilail akiangalia jinsi mtandao wa mazingira ulivyopangwa na utakavyofanyakazi baada ya kuuzindua rasmi kwenye ukumbi wa Mbayuwayu mbele ya wataalamu wa Mazingira kutoka nchi mbalimbali za Afrika na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Mtandao huu unapatikana kupitia

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates