DIAMOND PLATNUM: NATAKA KUWAPA AJIRA VIJANA WENZANGU


MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kupitia muziki huku pia akileta mapinduzi katika sekta hiyo nchini.

Diamond ambaye ni msanii ghali zaidi kwa sasa Tanzania, amesema kuna watu wengi wenye vipaji ambao wako mtaani au wako katika sekta nyingine lakini hawajui wafanyeje ili kufikia ndoto zao jambo ambalo linahitaji watu wengine wawasaidie kuwafikisha pale wanapotaka.

“Kuna tatizo ambalo lipo katika mambo ya mitindo, muziki. Watu wengi wanachukulia kama uhuni, wengi wanaona kama kuuza sura, yaani mtu aonekane kwenye video ili apate umaarufu, tunatakiwa kubadilisha mawazo haya, Ulaya hata hapo Afrika Kusini wanaonekana kwenye video wanalipwa.

  “Mimi nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa milango kwenye sekta nyingine, wapo wanaoweza kuonekana wanafaa kwenye matangazo ya biashara, hawa watapata kampuni ambazo zinaweza kuwatumia.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post