SIGOMBEI URAIS MIMI TENA ZITTO ABAINISHA

Naibu katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Zitto Kabwe hapo jana amewaondelea shaka wakazi wa Kigoma kwa kuwathibitishia kuwa atagombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uchaguzi na amewathibitishia wakazi wa Kigoma kuwa atagombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2015

Kwa mara ya kwanza Zitto Kabwe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini alitangaza nia yake ya kugombea urais mwezi Machi mwaka huu na kuzua mjadala kwa wadau wa siasa lakini baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kigoma bado walikuwa hawaamini wakidhani ni porojo za kisiasa tu

Kufuatia shaka hiyo akiwa Kigoma Taasisi ya Meza ya Duara ilimuomba Zitto kuonana na viongozi wa Taasisi hiyo pamoja na wananchi wengine ili kuzungumza nae kwa lengo la kumuuliza maswali juu ya masuala mbali mbali likiwemo la yeye kugombea urais ambapo Zitto amesisitiza nia yake hiyo


Amesema viongozi wa kizazi kilichotangulia Umetimiza wajibu wao kwa nchi na kwamba ni jukumu la kizazi cha sasa kuanzia pale walipoifikisha na kuisogeza nchi mbele zaidi inapotakiwa kuwa ambapo pia ameweka wazi kuwa atagombea kupitia CHADEMA na sio chama kingine.

Hata hivyo Zitto Kabwe amesema si jambo la lazima kwamba liwalo na liwe yeye kuwa rais bali itategemea na ridhaa ya wananchi wa Tanzania.



About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia