Wasanii wa kundi la muziki wa kizazi kipya bongofleva Wanaapolo la Mji
mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kutoka kushoto ni
Ramadhan Ally (Maimun) Ramadhan Mussa (Kize Bize) na Omary Michael
(Ben Lee)
WASANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya wa mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Wanaapolo wameibuka upya baada ya
kurekodi wimbo wao uitwao Sinyorita kwenye studio za Sharobaro Records
chini ya Producer Bob Junior.
Wanaapolo ambao ni wasanii maarufu wenye uwezo mkubwa wa kumiliki jukwaa
wanatarajia kutoa album yao yenye nyimbo nane itakayoitwa Sinyorita
ambayo itarekodiwa kwenye studio tofauti za jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa meneja wa Wanaapolo,Shamila Ramadhani kundi hilo
linasimamiwa kazi zake na Club Delux Mapipa ya mji huo chini ya
Mkurugenzi wake Mohamed Issa (Uspime) na Thadey Chusa.
Shamila alisema kundi la Wanaapolo linaundwa na wasanii wanne ambao ni
Ramadhan Ally (Maimun) Ramadhan Mussa (Kize Bize) Omary Michael (Ben
Lee) na Issa Amos (Wa2b).
“Baadhi ya nyimbo zitakazounda albamu ya Sinyorita ambazo zinatarajiwa
kurekodiwa hivi karibuni zaidi ya Sinyorita yenyewe ni Homa ya
mapenzi,Kazimika na Kinyulinyuli,” alisema Shamila.
Alisema hivi sasa kundi hilo linaendelea na mazoezi makali mji mdogo
wa Mirerani kwenye ukumbi wa Delux Mapipa ili baada ya mwezi huu
waanze kufanya matamasha mbalimbali hapa nchini.
“Kundi la Wanaapolo limepata umaarufu mkubwa hapa nchini kutokana na
stahili yao ya kushambulia jukwaa kwa umahiri mkubwa na wa hali ya juu
uliowawezesha kujulikana sehemu mbalimbali,” alisema Shamila.
Alisema kuwa wasanii wote wa kundi hilo ni wazaliwa wa mji mdogo wa
Mirerani kwenye machimbo maarufu ya madini ya Tanzanite ndiyo sababu
wakajiita jina la wanaapolo.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia