SIMBA YALAZIMISHWA SARE YA BAO MOJA KWA MOJA NA TIMU YA SON SUGAR YA NAIROBI


SIMBA SC leo imejikuta ikitoka  sare ya 1-1 na Son Sugar ya Nairobi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha , katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Katika mchezo huo,  Komabil Keita alijifunga katika jitihada za kuokoa na kuwapa Wakenya bao la kwanza katika dakika ya 42 huku bao la Simba lilifungwa na Daniel Akuffo katika dakika ya 60.
Awali, Simba ilicheza mechi mbili Arusha, dhidi ya Mathare United ya Kenya na JKT Oljoro ya Arusha, ambazo zote ilishinda 2-1, mshambuliaji mpya Daniel Akuffo kutoka Ghana akifunga bao moja kila mechi, Kiggi Makaasy na Mrisho Ngassa wakifunga mabao mengine.   
Simba inajiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kukutanisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.

Pia timu hii ya simba inatarajia kuondoka jijini Arusha ambapo imeweka kambi yake September nne mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao  ya ngao ya hisani .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post