Mariedo kuwavika magauni, viatu vya kisasa
MALKIA
atakayetwaa taji la Redd’s Miss Temeke 2012 katika shindano linalofanyika Ijumaa
Sept 21 katika ukumbi wa PTA(SabaSaba Hall), atajinyakulia zawadi zinazofikia
milioni 1.5 sanjari na tiketi ya moja kwa moja kushiriki shindano la Redd’s
Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
Katika
mlolongo huo wa zawadi, mshindi wa kwanza atajinyakulia fedha taslim Sh.
Milioni 1. Mshindi wa pili atajinyakulia fedha taslim Sh.laki nane wakati
mshindi wa tatu atapata Sh. Laki saba na washindi wote watatu kila mmoja
atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na viatu, vikiwa na thamani ya kila
mmoja Sh. Laki 5.
Duka
la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu cha Sh
150,000 kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda. Mbali ya
washindi hao, mshindi wa nne atajinyakulia kitita cha Sh. 400,000 ambapomshindi
wa tano ataondoka na Sh 300,000 wakati
warembo wengine wote watakaosalia kila mmoja atapata Sh.200.000.
Ikiwa
ni funga dimba ya mashindano ya urembo ya kanda nchini, shindano hilo
litanogeshwa na wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed
Original na Steve Nyerere ambaye mbali ya kuigiza sauti za watu mbalimbali, pia
ametoa filamu kadhaa kwa siku za hivi karibuni.
Mbali
ya wasanii hao, bendi ya Mashujaa Musica,yenye wanamuziki nguli kama Charles
Baba, MCD, Ferguson, Ali Akida sanjari na wanennguaji kama Lilian Internet na
wengineo pia itanogesha usiku huo.
Taji
la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss
Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji,
ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke
akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki wa mwaka jana Joyce
Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo wamekuwa na Dickson Daud
kutoka kundi la THT.
Shoo
ya ufunguzi itakuwa tofauti kabisa na shoo nyingine yeyote iliyowahi kuyanyika
nchini, kwani imezingatia zaidi urembo na nini msichana anatakiwa kufanya na si
unenguaji tu. Warembo 15 wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na
Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa
kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo
hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine
Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph,
Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam
Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali
ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo,
Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe
General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's
FM.
Temeke
imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness
Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na
Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili
na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene
Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda
Kalikawe na Asela Magaka.