Katikati ni mshindi wa Redds Miss Lake zone 2012/13 Eugene Fabian kutoka Mara akiwa katika sura ya furaha mara baada ya kutangazwa rasmi kunyakua taji hilo, Kushoto kwake ni mshindi wa Tatu Happiness Rweyemamu kutoka Shinyanga na Kulia kwake ni mshindi wa pili Happiness Daniel kutoka Mwanza. Washindi hawa watatu watawakilisha Kanda ya ziwa katika shindano la taifa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao. Mshindi wa kwanza ameondoka na kitita cha shilingi Laki 7, mshindi wa pili laki 5 na mshindi wa tatu laki nne na nusu
Tatu bora wakiwa wamepozi kwa raha zao.