Kutokana
na uharibifu wa eneo la hifadhi ya maji ya mto Eyasi ulioko Wilayani Karatu
unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wa eneo hilo kuendelea kwa muda mrefu, Mkuu wa wilaya
hiyo ametoa Amri ya wawekezaji hao kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo
kufukuzwa.
Akiongea
kwenye mkutano mkuu wa hadhara na wananchi wa Tarafa ya Eyasi, mkuu wa wilaya
ya Karatu Daudi Ntibenda Kijiko alitoa amri hiyo baada ya kufanya ziara ya
kutembelea hifadhi ya maji ya mto huo na kukuta uharifu mkubwa uliofanya na baadhi ya wawekekezaji
wa eneo.
Awali wakati wa kutembelea
hifadhi hiyo wananchi wanaozunguka hifadhi walisema kuwa, wamekuwa wakionewa na
watu hao na hata kutishiwa maisha pindi wakiwakataza kuharibu vyanzo hivyo vya
maji hali inayahatarisha usalama wao kwa sasa na hata baadae endapo chanzo
kikikauka.
Mwananchi mmoja
aliyejitambulisha kama Yusuphu Abdi mkazi wa Mang’ola alisema kuwa maji ya
chanzo cha mto Eyasi ndio tegemeo kubwa kwao kwa matumizi ya kawaida ya
nyumbani, na kiuchumi kwa kuyatumia kumwagilia mazao yao ya kilimo hasa vitunguu ambacho kimekuwa
chanzo kikubwa cha kipato chao.
Alisema kuwa kwa sasa hawana
matumaini tena na maji hayo baada ya watu hao kuvamia chanzo hicho cha maji na
kukata miti, kuchoma misitu, pamoja na kujenga mabanda ya kuikia wageni( kempu)
pamoja na vyoo juu ya vyanzo hivyo wakati wananchi wanategemea maji hayo kwa
matumizi ya nyumbani ikiwemo kunywa.
Baada ya ziara hiyo ya
kutembelea hifadhi hiyo ya maji na kujionea uharibifu mkubwa uliofanywa na watu
hao huku ikihatarisha usalama wa vyanzo hivyo vya maji kuendelea kuwepo ambapo
alifanikiwa kuwakamata watu ambao ni baadhi ya waharibifu wa vyanzo hivyo vya
maji baada ya kuhudhuria kwenye mkutano huo.
Ntibenda alisema kuwa jukumu
la kutunza mazingira ni la kila mtu bila kujali mgeni au mwenyeji hivyo hivyo
haiwezekani kuwavumilia baadhi wa watu wanaojifanya miungu watu kwa
kujitajorisha wenyewe na kuwauwa wananchi kwa kuharibu chanzo hicho cha maji
kwa manufaa yao
binafsi na kuwanyima wananchi.
“Haiwezekani kuendelea
kuwavumilia watu wachache wasio na utu hadi kupeleke kuvamia eneo la hifadhi ya
maji na kuharibu vyanzo vya maji na kufunga bendera nyekundu kuashiria umwagaji
wa damu, hii ni kupima nguvu ya serikali iko wapi hali ambayo hatutavumilia
hivyo wananchi tushirikiane hata katika siku ya kuchoma makempu yaliyoko eneo hilo” alisema Ntibenda.
Baada ya kukamatwa kwa
watuhumiwa hao wananchi wa Tarafa hiyo waliiomba serikali kuwachukulia watu hao
hatua kali za kisheria ili kunusuru chanzo hicho kwa kutorudia kuvamia tena na
kuharibu kwani mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na kuachiliwa na mahakama ya
mwanzo ya mang’ola hali iliyopoteza imani na hakimu wa mahakama hiyo.
Ziara hiyo ya mkuu wa wilaya
ya Karatu pia iliwahusisha mb’unge wa jimbo la Karatu Israel Natse, wakuu wa
idara mbalimbali wilaya ya Karatu pamoja na jeshi la polisi na wanahabari.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia