BREAKING NEWS

Monday, September 10, 2012

TAZANIA KUPUNGUZA KEMIKALI ZA TABAKA LA ORIZONI KUTOKA TANI 254 HADI TANI 36.2 KWA MWAKA

Waziri wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais Dkt,Terezya Huvisa katikati akiwa anaongea na waandishi wa habari jijini hapa leo kuhusiana na siku ya maadhimisho ya kitaifa  ya hifadhi ya tabaka la ozoni  wa kwanza kuliani ni naibu waziri wa mazingira Charles Kitwanga

 washiriki wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa manyara uliopo ndani ya jengo la mikutano la AICC
Charles Kitwanga naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais mazingira akiwa nafafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kushoto ni waziri wa mazingira
TANZANIA imefanikiwa kupunguza matumizi ya kemikali zinazomong'onyoa tabaka
 la hewa la orizon angani kutoka tani 254 kwa mwaka hadi kufikia tani 36.2 sawa na asilimia 86 huku ikiwa ni nchi ya kwanza kwa bara la Afrika kuweza
kufikia malengo yake kwa kiwango kikubwa ingawaje bado kuna changamoto
 kubwa hasa kwenye majokofu na viyoyozi.
 Hayo yalielezwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira dr
Terezya Huvisa wakati alipokuwa akiongea katika mkutano wa baraza la
 mawaziri wa mazingira kwa nchi za Afrika mapema jana jijini hapa.

Dr Terezya alisema kuwa tanzania imefanikiwa kufikia hatua hiyo ktokana na

juhudi mbali mbali ambazo zinafanyawa na wizara yake kwa kushirikiana na
taasisi nyingiena hali ambayo imetoa sifa kubwa sana kwa nchi za bara la
afrika na kusababisha kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimepunguza madhara ya
 tabaka la ozoni.

"kama tunavyojua ozoni ni hewa iliyoko kwenye anga hewa juu takribani

kilomita 10-50 juu ya ardhi na kwa hali hiyo tabaka la ozoni
 linapoharibuiwa uchangia kuruhusu mionzi zaidi kufika kwenye uso wa dunia
na ndio maana kuna ongezeko kwa magonjwa mbali mbali kama vile saratani ya
 ngozi ,uharibifu wa macho,kwa hali hiyo sisis tumepiga hatua kubwa sana
 kuliko nchi nyingene barani afrika "alisema dr Terezya.

Pia aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo ya nchi ya tanzania kuwa miongoni

 mwa nchi zilizopiga hatua kwa zaidi ya asilimia 86 ya kupunguza kasi hiyo
 ya kemikali alisema kuwa mnamo septemba 16 mwaka huu tanzania itaungana na
 jumuiya ya kimataifa ya kuazimisha siku ya hifadhi tabaka la ozoni ambapo
 mgeni rasmi ambaye ni makamu wa rais atakabidhiwa tuzo kama mshindi wa
 kwanza wa kupoambana na tabaka la hewa ya ozoni .

Alifafanua kuwa makamu wa rais atapewa zawadi hiyo kama mshindi wa kwanza

 miongoni mwa nchi zote za bara la afrika ambapo kutokana na tuzo hizo
 zitachangia kwa kiwangi kikubwa kwa watanzania kuweza kupunguza na kepukana
na vifaa mbali mbali ambavyo vinacdhangia kukithiri kwa kemikali hiyo
 ambayo ina madhara makubwa sana kwa maisha ya kawaida .

Wakati huo huo waziri huyo alisemam kuwa miongoni mwa changamoto nkubwa

 ambayo wanayo ni pamoja na changmaoto ya matumizi ya majokofu na viyoyozi
ambapo baadhi ya vifaa hivyo vinachangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo
kwa gesi ambayo ndio chanzo cha magonjwa mbali mbali pamoja na uharibifu wa
mazingira.
 Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni vema kama watanzania wakahakikisha
kuwa wanafuata taratibu mbali mbali ambazo zinatolewa na serikali ikiwa ni
 pamoja na kuachana na kununua vifaa ambavyo vimetoka nnje ya nchi (mitumba)
 ambapo baadhi yake ndivyo vyenye gesi yenye madhara kwa binadamu.
 "nawasihi sana watanzania wezangu kuepuka  kutupa ovyo majokofu ya zamani
 ama vifaa vya kuzima moto vyenye kemikali zinazomongonyoioa tabaka la ozoni
aina ya CFCs na halon bali hakikisheni mnapata ushauri wa kitaalamu kutoka
kwa mafundi ama mamlaka zinazousika"alisisistiza

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates