Ticker

6/recent/ticker-posts

SEREKALI YATAKIWA KUBADILISHA MFUMO WA UZAJI VYUMA CHAKAVU

Meneja wa tanesco mkoa wa Arusha Nekoluaus kamoleka akimkabidhi diwani wa kata hiyo Ernest Pendaeli fedha kwa ajili ya kuwapa wanachi waliofanikisha kukamatwa kwa mwizi wa waya za shaba za umeme
Shirika la umeme tanesco mkoa Arusha limeitaka serikali kubadilsha mfumo wa uzajia wa chuma chakavu kwani inapelekea shirika hilo kupata asara ya shilingi million mia tano kwa kila mwaka kwa waya aina ya shaba kuibiwa na kuuzwa kwa watumiaji wa chuma chakavu .

Ayo yamesemwa na meneja wa shirika la umeme mkoa arusha bwana Nekoluaus Kamoleka   wakati akikabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa wananchi wa kijiji cha nkwamakasha  mkoani arusha kwa kumkamata jambazi aliyeiba nyaya za shaba katika eneo hilo aliyefamika kwa jina la bakari saidi

Alisema kuwa tanesco imekuwa ikingia hasara kubwa na pamoja nakurudi nyuma katika maendeleo kwani kumekuwepo na tatizo kubwa la wizi wa waya za shaba katika maeneo mengi.

Alisema kuwa biashara hii ya vyuma chakavu imefanya shirika hili kuingia hasara kila mwaka kwani wananchi wamekuwa wakiiba nyaya hizi za shaba kwa ajili ya kwenda kuuza ili wapate hela hivyo ameitaka serekali kuzuia biashara hii   na ikishindikana kujitaidi kuthibiti biashara hii kwani imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.

"wananchi wamekuwa wakikata nyaya hizi na kuzichukuwa na kwenda kuuza ,na wanapouza wanauza bei gali sana kwani tulivyomuhoji mwizi huyu ambaye tumemkamata alisema kuwa kila kilo moja ya wanya huu wa shaba wamekuwa wakiuza kiasi cha shilingi elfu kumi hivyo bei hii ndo inawashawishi kuiba nyaya hizi sasa kibaya zaidi wezi hawa wamekuwa wakikata nyaya hizi hata kukiwa na umeme kitu ambacho kinawahatarishia hata maisha yao wenyewe"alisema Kamoleka

Alitoa wito kwa wananchi kuwa walinzi kwa wenzake na pindi atakapo mjua mwizi wa waya hizi na hata wa umeme ato taarifa polisi au hata katika ofisi ya tanesco iliyopo karibu nae kwani wakiwafichia siri wanapelekea kuendelea kuletea shirika hili hasara kwani badala ya kusonga mbele kuendelea kuwafungia wananchi wengine umeme watakuwa wanarekebisha sehemu ambazo waya hizo zimekatwa kitu ambacho kinawaletea hata shida wananchi kwa kuchelewa kufungiwa umeme.


Meneja huyo wa tanesco mkoa wa Arusha alibainisha kwamba kwa kushirikiana na jeshi la polisi mtuhumiwa huyo wa wizi wa miundo mbinu ya tanesco atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ivyo ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kuwakamata wezi hao wa nyaya za umeme

Akiongea na libeneke la kaskazinidiwani wa kata hiyo Ernest Pendaeli  alisema kuwa wamekua wakikosa maendeleo ya uzalishaji kwa muda mrefu kutokana na uwizi wa mara kwa mara unaotokea katika kata yake ambapo wamekua wakishindwa kufanya uzalishaji wa mashine mabli mbali

Diwani pendaeli alisema kua vijana wa kata hiyo wameonyesha mfano mzuri wa kuweka doria na kukesha kuwatafuta waalifu hao wa wizi wa nyaya hizo hadi kufanikiwa kuwakamata napia wameipongeza shirika hilo kuwapatia fedha hizo za asante kwa ushirikiano wao na tanesco.

Post a Comment

0 Comments