SUPER SPORT YAITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KATIKA MEDANI YA MICHEZO KWA KUZINDUA WIKI YA SOKA TANZANIA
Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akifafanua ujio wa
Super Sport nchini Tanzania na kuipongeza TFF kwa kuonyesha ushirikiano
na kuwa Chaneli hiyo itaonyesha mechi tano za Ligi ya Tanzania kuanzia
leo Ijumaa Septemba 28 hadi Jumatano Oktoba 3 mwaka 2012
Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Leordiga Tenga
akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Soka Tanzania ambapo
amevitaka vilabu vitakavyopata bahati ya kuonekana katika chaneli hiyo
kuonyesha kiwango cha soka la Tanzania na kuzingatia nidhamu haswa mechi
ya Watani wa Jadi Yanga na Simba ambao wanatambulika barani Afrika kama
timu zenye upinzani mkali.
Mkuu wa Super Sport barani Afrika Bw. Andre Venter akielezea furaha yake
kuja Tanzania na kupata fursa ya kulitangaza soka la Tanzania kimataifa
kupitia chaneli ya Super Sport amesema chaneli hiyo imechafanya kazi
katika nchi za Kenya na Uganda na Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha
kiwango chake cha soka Kimataifa.
Baadhi ya Wadau wa michezo wakipata viburidisho wakati wa uzinduzi wa wiki ya soka Tanzania
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo kuwa Super Sport
wakishirikiana na TFF wapo hapa nchini na kwa mara ya kwanza wanaonyesha
mechi za Ligi ikiwemo timu ambazo hata siku moja hazijawahi kuonekana
kwenye Chaneli ya Super Sport na kuwataka wachezaji wa timu hizo
kuonyesha uwezo wao kwa sababu ni fursa ya pekee kuonekana katika nyanja
ya Kimataifa. Aidha amewataka Watanzania ambao hawajaunganishwa na DStv
wafanye hima kununua ving'amuzi ili waweze kushuhudia mechi hizo pamoja
na chaneli nyinginezo zinazopatikana katika DStv
Kipindi cha Africa Soccer Show kwa mara ya kwanza kilifanyika LIVE
nchini Tanzania. Pichani ni Watangazaji wakifanya mahojiano na Katibu
Mkuu wa TFF Bw. Angetile Oseah (katikati).






0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia