BREAKING NEWS

Tuesday, September 18, 2012

MKUTANO MKUU WA WAANDISHI WA HABARI WAFANYIKA MTO WA MMBU SAMBAMBA NA ZIARA YA HIFADHI YA TARANGIRE

 waandishi walifurahia sana safari hii hapa ndipo walipowasili katika eneo la mapokezi la hifadhi ya Tarangire
 mara baada ya kuingia katika lango au mapokezi ya hifadhi ya tarangire mwana dada wa libeneke alipiaga picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari  wa kwanza kulia ni mwanadada Mary Mwita mwandishi wa habari wa gazeti la mtanzania wa pili ni mdada Cithia mwilolezi wa gazeti la nipashe  na wa kwanza kulia ni mdada anaye ripotia tv ya clouz fm betrece jeradi
 hawa ni wanyama haina ya Ngiri wapo ndani ya hifadhi hii
 hapa tulipoingia katika hifadhi ya Tarangire tulipata somo kwanza linalohusiana na hifadhi hii


 kwenye chakula cha mchana pia tulikutana na wageni wengi waliotembelea hifadhi ya tarangire hapa wanabadilishana mawazo hii yate ni utalii
 Tumbili akinywa juice ndani ya hifadhi
 hhi ni mida ya misosi ndani ya hifadhi ya tarangire
 tumbili akiwa anamnyonyesha mtoto wake ndani ya hifadhi ya tarangire
 hawa ni nyumbu
 Wakili maarufu hapa nchini Mawala akiwa anatoa mada ya sheria za wanyama pori mara baada ya waandishi kumaliza ziara yao ya kutembelea hifadhi ya Tarangire

 wengine walikuwa wanafatilia mechi ya livepool
 wengine hawana hobi ya kucheza kwanja waliendelea kupata kinywaji
 kwanja kaka acha tu hii yote ni TANAPA imesababisha

 mwenyekiti wa APC Claud Gwandu akisoma hutuba fupi ya mgeni rasmi
 washiriki wakiwa wanasikiliza kwa makini
 mkuu wa wilaya ya monduli  Jowika Kasunga akiwa anafungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa arusha  mkutano uliofanyikia mjini mto wa mmbu
 Mkuu wa wilaya ya monduli akiwa na mweka hazina wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa arusha wakijaribu kufungua nembo ya chama hicho ambayo ilizinduliwa rasmi siku ya mkutano mkuu wa chama
mkuu wa wilaya ya monduli akiwa anampa mkono mwenyekiti wa chama cha APC mara baada ya kumaliza kuzindua nembo ya chama


 waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkuu wa wilaya ya monduli kufungua mkutano
mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga amelaani vikali mauaji ya muandishi wa habari wa chanel Ten Daudi Mwangosi yaliyofanywa na polisi hivi karibuni mkoani Iringa wilayani nyololo.

Alitoa kauli hiyo  wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoani Arusha (APC) uliofanyika katika ukumbi wa Transit ulipo   mto wa mmbu wilayani monduli

Alisema kuwa mtu yeyote mwenye akili timamu awezi kuchekelea mauaji ya mwandishi huyo isipokuwa ni lazima tukemee ili yasifanyike tena na kuyalaani vikali

Alibainisha kuwa nchi ya tanzania ni tulivu na inaamani lakini watu wachache wanataka kuiletea nchi hii vita kitu ambacho ni hatari sana kwa wananchi.

kwa upande wake mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha Claud Gwandu alisema kuwa wao kama chama cha waandishi wa habari mkoa wa aruha wamelaani vikali mauaji haya ya mwandishi na sio mwandishi tu bali pamoja na wananchi wengine ambao wameuwawa  pasipo kuwa na sababu

Alibainisha kuwa askari wamekuwa wakitumia silaha zao sivyo kwani  badala ya kutumia silaha zao kuwalinda wananchi wamekuwa wakiwauwa kwa kutumia silaha hizo

"unajua silaha hizo zinatakiwa kuwalinda wananchi pamoja na wanahabari wakiwepo kazini badala ya kukiuka na kuwaua na pia kwanini wawauwe wananchi wasio na hatia wakati kuna wahalifu "alisema gwandu

Aliongea kuwa bila amani ya nchi hakuna haki ,maendeleo hayata kuwepo na tukiwa hivyo tutakuwa kama wananchi wa somalia ambao nchini kwao kunavita na hawaishi na amani wanakimbia kimbia katika nchi mbalimbali.

Aliwataka wanasiasa ,viongozi ,wananchi pamoja na polisi kuendeleza amani ya nchi yetu ili historia ya amani iendelee kudumu hapa nchini

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates