CUF WAIHUSISHA CHADEMA NA VURUGU ARUSHA
CHAMA
Cha Watu wananchi CUF kimetoa tamko kali kwa kuwatuhumu wafuasi sita wa
Chadema jijini Arusha kwamba walihusika na vurugu za kulishambulia gari
la matangazo na kisha kumpiga mawe mfuasi wao huku wakilitaka jeshi la
polisi kuchukua hatua kali za kisheria.
Akitoa
tamko hilo,jana katika ofisi za chama hicho zilizopo kata ya Kaloleni
jijini Arusha,mjumbe wa baraza kuu la uongozi taifa wa cuf,Mbarala
Maharagande alisema kwamba chama chao kina ushahidi wa kutosha kwamba mfuasi wao ,Athuman Abdulraham alipigwa mawe na wafuasi wa Chadema wakati akiwa katika gari la matangazo.
Maharagande,alisema
kwamba mfuasi wao alikuwa katika eneo la Levolosi karibu na eneo
lililovamiwa na wamachinga na wakati akiwa ndani ya gari hilo wafuasi wa
Chadema walianza kumyooshea alama ya vidole viwili kabla ya kuanza
kumpopoa kwa mawe.
Hatahivyo,alisisitiza
kwamba tayari mfuasi huyo ameshatoa tarifa kwa jeshi la spolisi mkoani
hapa na kufungua faili nambari AR/RB/12419/012 na kulitaka jeshi hilo
kuwakamata wafuasi hao wa Chadema hadi kufikia septamba 30 mwaka huu na wakishindwa wao watachukua hatua za kisheria wanazozijua.
“Kijana
amepigwa na wafuasi wa Chadema na tayari tunawajua wako sita tumeshatoa
tarifa polisi wawachukulie hatua na kama wakishindwa basi sisi
tutachukua hatua za kisheria tunazozijua”alisema Maharagande
Alisema
kwamba wana tarifa za kutosha kwamba Chadema wamefanya vurugu za kutaka
kuharibu mkutano wa hadhara wa chama chao unaotaraji kuhudhuriwa na
mwenyekiti wake,Prof Ibrahim Lipumba sanjari na makamu mwa kwanza wa
Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad .
Alisema
kwamba wao wamekuja Arusha kufanya kazi za siasa zikiwa ni pamoja na
kujiandaa na uchaguzi wa madiwani,ubunge pamoja na kueneza será ya V4C
iliyoasisiwa hivi karibuni.
Hatahivyo,alisisitiza
kwamba wao hawapendi kupambana na Chadema kwa kuwa hawana serikali huku
akisisitiza kuwa kama ni fujo wanazijua lakini kwa sasa wanaeneza será
na kama Chadema wakitaka kupambana nao wakashindane kwa hoja majukwaani.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia