FJAJI MFAWIDHI ATAKA WANANCHI WAJITOKEZE KWA WINGI KUTOA MAONI YA KATIBA MPY

wanasheria mawakili wafanyakazi wa kituo cha haki za binadamu wakiongonwa na jaji Aisha nyerere wakiwa katika maandamano ya kuathimisha miaka 17 ya kuanzishwa kwa kituo cha sheria na haki za binadamu maathim misho yaliyobebwa na kauli mbiu usemayo kuwalinda kuwatetea watetezi wa haki za binadamu tanzania ni wajibu watu sisi,maadhimisho yaliyofanyikia jijini arusha
jj jaji aisha nyerere akiwa anasoma hutuba katika maadhimisho Jaji Aisha Nyerere Akisoma risala katika s

jaji Aisha nyerere akiwa anazindua vitabu viwili kimoja kikiwa kinajulikana kwa jina la wajibu wa makampuni huku kingine kikiwa kimeandikwa kampuni ina wajibu wa kufanya shughuli zake kwa kuzingatia kulinda kuendeleza na kuheshimu misingi ya haki za binadamuvitabu vyote hivyo vilizinduliwa janakwenye maadhimisho hayo
Add caption

kikundi cha ngoma cha laleti kikitumbuiza

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,  Aisha Nyerere, amewataka
wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni kuhusu mambo wanayoyataka
kwenye Katiba Mpya.
Aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati akizindua
vitabu vya uwajibikaji wa makampuni kwa jamii pamoja na kitabu kinachohusu
haki za jamii katika maeneo ya uwekezaji, uzinduzi ulioenda sambamba na
maadhimisho ya miaka 17 ya Kituo cha Sheria na Haki Bbnadamu (LHRC).
“Napenda niwakumbushe Watanzania kuwa kwa sasa taifa letu lipo katika
mchakato wa kutunga Katiba mpya, mchakato huu upo katika hatua za mwanzo
kabisa ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi,hivyo kwa kuzingatia hayo napenda
kuwahimiza ninyi na raia wengine kushiriki kikamilifu kikamilifu kutoa
maoni yenu.
“Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu pamoja na watu wengine wenye nafasi
na uwezo wa kutoa elimu kwa umama kushiriki kikamilifu katika mchakato
mzima, mnapaswa kutumia vema nafasi zenu,” alisema.
Alisema watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakikumbana na
changamoto mbalimbali hivyo wanapaswa kuungwa mkoni kwani utetezi wa haki
za binadamu ni wajibu wa jamii nzima.
“Watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuisaidia serikali katika
uendelezaji na kulinda haki za binadamu na ni nafasi pekee kutengeneza
misingi imara ya kuwatetea na kuwalinda watetezi wa haki za binadamau na
kuna nafasi nzuri kama wakati huu wa mchakato wa kuhakikisha kuwa haki za
binadamu na matamko mbalimbali ya kimataifa yanaridhiwa na kuwekwa katika
katiba mpya kwani hii itakuwa na mchango mkubwa sana katika kulinda haki za
binadamu na watetetzi wa haki hizo,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Hellen  Kijo Bisimba,
alisema baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa ziliwakabili katika
kutekeleza majukumu yao ni pamoja na sheria kwua kandamizi, hata wanapokuwa
wanapokuwa wanamsaidia mtu kisheria, sheria zimekuwa zikiwakandamiza.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la mfumo wa mahakama ambapo
mashauri yamekuwa yakichukua muda mrefu hadi kukamilika,wasaidizi wa
kisheria kutokutambulika.
Dk. Hellen aliongeza kuwa vyombo vya dola navyo vimekuwa ni tatizo kwao
kwani wakati mwingine wao wakiwa katika majukumu yao ya utetezi,vyombo vya
dola vimekuwa vikiwaona wao ni wapinzani wakati wao ni wasaidizi wa
serikali.
Naye Mratibu wa Kitengo cha Uwajibikaji wa Makampuni na Mazingira cha
kituo hicho, Wakili Flaviana Charles, akizungumza wakati wa uzinduzi
wa vitabu hivyo
alisema kuwa  sheria ya uwekezaji hapa nchini haina vifungu vyenye kutoa
wajibu wa wawekezaji kwa wananchi jambo linalosababisha jamii kutokunufaika
na miradi ya uwekezaji inavyotekelezwa katika maeneo husika.
Aliongeza kuwa ukosefu wa sheria inayosimamia uwajibikaji wa makampuni kwa
jamii umepekelea kuwepo kw augumu wa kuzichukulia hatua za kisheria kampuni
zinazoshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii,ambayo imesababisha uwepo kwa
migogoro isiyoisha ndani ya jamii.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post