WAALIMU wanaofundisha somo la Hisabati kote nchini wametakiwa kutafuta mbinu mbadala za kufundisha somo hilo kwa wanafunzi ili kuwatia moyo na kufanya walipende somo hilo ,kwani kumekuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi kutofaulu vizuri kutokana na walimu kutokuwa na mbinu sahihi za kufundishia.
Hayo yalisemwa jana na Naibu waziri wa elimu Tamisemi Kassimu Majaliwa katika hotuba yake iliyosomwa na Mkaguzi mkuu wa elimu kanda ya kaskazini,Kapombe Mzava katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha hisabati Tanzania (MAT CHAHITA)uliwashirikisha waalimu wa somo la hisabati kutoka vyuoni,shule za msingi na shule za sekondari kutoka mikoa yote ya Tanzania uliofanyika katika chuo kikuu cha Mkumira kilichopo mjini hapa.
Alisema kuwa,upo umuhimu kwa walimu kubuni mbinu mpya za kuwavutia wanafunzi ili wajijengee moyo wakupenda somo la hisabati kwani kiwango cha ufaulu katika somo hilo kimekuwa kikiendelea kushuka siku hadi siku, hivyo lazima walimu sasa watafute ufumbuzi wa tatizo hilo.
Alisema kuwa, ufaulu wa somo la hisabati kwa shule za msingi kwa mwaka jana lilikuwa asilimia 14 ambapo kiwango hicho kinasikitisha sana , hivyo ni lazima kila mmoja aweke nguvu za pamoja kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanavutiwa na somo hilo.
Aidha aliwataka walimu hao kukaa chini na kujadili chanzo cha kufeli kwa wanafunzi katika somo la hisabati kwani kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakienda darasani kwa vitisho hatua ambayo hupelekea wanafunzi kukimbia somo hilo pindi linapofikia.
Naye Mwenyekiti wa chama cha hisabati Tanzania (MAT /CHANITA) , Dk.Sylvester Rugeihyamu alisema kuwa, mkutano huo ni wa 47 tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1966 ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka kuwakutanisha walimu wanaofundisha somo la hisabati Tanzania kwa lengo kuboresha ufundishaji wa somo hilo sambamba na kutafuta ufumbuzi unaosababisha kiwango cha ufaulu wa somo hilo kichuka.
Alisema kuwa, dhumuni kubwa la kuwaunganisha wataalamu wa hisabati kote nchini ni kubadilishana ujuzi uzoefu na hivyo kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisababti na matumizi yake katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa, mbali na kuzungumzia mbinu mbalimbali za kuboresha ufundishaji katika somo hilo la hisabati ,wametoa wito kwa serikali kuondoa mfumo uliopo sasa unaotumika kutunga mtihani wa somo hilo kwa wanafunzi kuchagua majibu badala ya kufanyakazi ya kukokotoa na kutoa jibu.
Alifafanua kuwa hatua hiyo imechangia kwa kiwangi kikubwa wanafunzi kupunguza kiwango cha ufaulu kwani majibu wanayoyatoka kwenye karatazi za mtihani ni ya kubahatisha na si yaye ya kufanya kazi.
Wamelishauri baraza la mtihani Tanzania kubadili mfumo huo kwani hatua hiyo haibanishi uwezo sahihi wa mwanafunzi katika hisabati badala yake inatoa mwanya mkubwa kwa mwanafunzi kubahatisha .
‘Unajua sisi tunaoimba serikali iondoe mfumo huo kwani umekuwa ukiwasababishia wanafunzi kuwa mbumbu na kutokuwa na uwezo wa kufikiri kutokana na kubahatisha majibu, hivyo tunaomba mtihani wa somo la hisabati ufanyike kwa kuonyesha njia na majibu na kwa kufanya hivyo wanafunzi wataweza kuwa na uelewa mpana wa kufikiri’alisema Dk. Rugeihyamu.
Aidha alitaja changamoto zinazokabili chama hicho kuwa ni pamoja na ukosefu wa fedha za kutosha ili kuendesha shughuli za chama ,pamoja na waajiri kutokuwa tayari kuwawezesha waalimu kuhudhuria semina na warsha za MAT/CHAHITA
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia