Raia wa Ugiriki,Sotiris Sotiriades (87)akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kulalamikia suala la kunyanyaswa na mamlaka ya kahawa ACU.
RAIA wa Ugiriki anaishi nchini Tanzania ,Sotiris Sotirades (87) ameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wake wa ardhi baina yake na mamlaka ya kahawa ya Arusha Cooperative Union Ltd (ACU) ambao umedumu kwa kipindi cha miaka 13 hadi sasa bila kupatiwa ufumbuzi wowote. Aidha katika mgogoro ACU inamtaka Sotirades kuondoka yeye na familia yake kwenye eneo lake lenye ukubwa wa heka 7 ambalo amekuwa akiishi tangu mwaka 1978 katika kijiji cha Chemchem, kata ya Usariver wilayani Arumeru ,baada ya kukabidhiwa kisheria na mmiliki wa awali, Maxton Mailer farm chini ya uongozi wa kijiji hicho .
Akizungumzia mgogoro huo , Sotirades ambaye ameishi nchini kwa zaidi ya miaka 62 alisema kuwa , yeye amekuwa akiishi na familia yake katika eneo hilo tangu mwaka 1978 , ambapo alishangazwa ilipofika mwaka 1999 kutakiwa kuondoka katika eneo hilo akidaiwa kuwa nyumba hiyo ni mali ya ACU.
Alisema kuwa ,baada ya watu hao kufika eneo hilo, alitaka kujua undani zaidi kuhusu swala hilo ndipo alipoelezwa kuwa, eneo hilo lilichukuliwa na serikali na kukabidhiwa ACU,hatua iliyomshangaza huku ikidaiwa kuwa yeye alikuwa mpangaji na si mmiliki.
Alifafanua zaidi,kipindi hicho viongozi hao wa ACU walikuwa wakiuza maeneo mengi yaliyokuwa yamepakana na eneo hilo na baada ya kumaliza kuuza ndipo walianza kudai eneo hili pia ni mali yao.
Alisema baada ya kuibuka mgogoro huo na yeye kugoma kuhama katika eneo hilo,mwaka 1999 ACU waliamua kukimbilia mahakamani wakidai wao ndio wamiliki halali wa eneo ,huku wakieleza ya kuwa mzee huyo alikuwa mpangaji wao.
'' baadae niligundua kuwa ACU walikuwa wamechukua fedha kwa mtu aitwaye Willy Aron Mushi kiasi cha shs milioni 200 kwa lengo la kumuuzia eneo hilo,''alisema
Alisema kuwa kesi hiyo ya madai namba 11 ya mwaka 1999 ilifunguliwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Arusha chini ya hakimu,devota Msofe na ilipofika mwaka 2005 hukumu ya kwanza ilitoka na mahakama ikaamuru raia huyo kubakia na umiliki wa eneo hilo.
Aliongeza kuwa, ACU walishindwa kuridhika na maamuzi ya mahakama hiyo na kuamua kukata rufaa mahakama ya juu, ndipo kesi ilipoendelea tena katika mahakama hiyo na hukumu nyingine ilikuwa mwaka 2007 ikimtaka raia huyo kuendelea kumiliki eneo lake.
Hata hivyo, mwaka huo ACU ilifungua kesi nyingine mahakama ya Ardhi mkoani hapa ikiwa haikuridhika na maamuzi ya mahakama zilizopita.
''ACU baada ya kushindwa mara mbili waliamua kufungua kesi hiyo mahakama ya Ardhi na lengo lao wanasubili nife ili weweze kulichukua eneo hilo kwani mimi sasa ni mzee sina uwezo mwengine zaidi ya kuiomba serikali ya Tanzania inisaidie''alisema
''ACU baada ya kushindwa mara mbili waliamua kufungua kesi hiyo mahakama ya Ardhi na lengo lao wanasubili nife ili weweze kulichukua eneo hilo kwani mimi sasa ni mzee sina uwezo mwengine zaidi ya kuiomba serikali ya Tanzania inisaidie''alisema
Alisema kuwa, kesi hiyo ilianza kusikilizwa katika mahakama ya ardhi mwaka 2007 chini ya hakimu Boniface Makombe ambapo hadi sasa hivi hakuna chochote kinachoendelea zaidi ya kuendelea kupigwa tarehe ambapo kesi hiyo itatajwa tena 23/10 mwaka huu.
Mzee huyo analalamika manyanyaso yanayofanywa na ACU dhidi yake wakitaka kumdhulumu kutokana na umri wake kuwa mkubwa, kwani ameshindwa hata kuliendeleza eneo hilo pamoja na kuikarabati nyumba yake ya kuishi,kwani hajui hatma ya kesi hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.
Pia ameiomba mahakama hiyo kuharakisha maamuzi ili ajue hatma yake kwani anahofia maisha yake kutokana na umri wake kuwa mkubwa kwani kwa sasa anaishi kwa tabu huku akidai fedha nyingi ametumia kwenye kesi hiyo huku familia na watoto wakimkabili .
Aidha raia huyo ambaye anaishi na familia ya kitanzania ambao amekuwa akiishi nayo kwa muda mrefu tangu amehamia katika eneo hilo na amekuwa akimsadia kusomesha watoto wake walioko chuo kikuu na wengine shule za msingi.
‘Jamani naomba serikali inisaidie kuingilia kati kwani watu hawa wanaendelea kusogeza tarehe mbele ili nifariki waweze kutapeli eneo hilo kwa urahisi , jamani naomba serikali inisaidie kwani nimeshatumia fedha nyingi sana hadi sasa hivi kwa ajili ya kuweka mawakili katika kushughulikia kesi hii kwani mimi sasa ni mzee nguvu hiyo sina’alisema Sotiris.
Hata hivyo aliiomba serikali kuwachunguza watu hao wanaodai kuwa ni viongozi kutoka ACU ambao wapo watatu ambao ni Clavery Mkwawa anayejiita meneja wa ACU, Laizer na Boni ambao wamekuwa wakijitambulisha kuwa wao ndio viongozi wa ACU.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia