Mabingwa
wa Tanzania bara Simba SC leo hii wameendeleza makali yao waliyoanza
nayo ligi kwa kuitandika timu ya wanajeshi wa JKT Ruvu kwa mabao mawili
kwa sifuri.
Simba
ambao walicheza mchezo kwa dakika nyingi baada ya mshambuliaji wao
tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza
cha mchezo, walipata mabao yao kutoka kwa kiungo Amri Kiemba aliyefunga
bao la kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga kidude cha pili.
Kufuatia
matokeo hayo Simba inaendelea kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya
pointi 6, magoli matano ya kufunga na wakiwa hawajuruhusu nyvu zao
kuguswa. Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa 3 - 0 dhidi ya
African Lyon.
Kwa
upande mwingine huko jijini Mwanza Azam FC wametoka sare ya kufungana
2-2 na Toto Africa, wakati Tanzania Prisons wamedungwa 1 - 0 na Coastal
Union ya Tanga, Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, huku
Ruvu Shooting wakiifunga Mgambo JKT 2-1.