SEREKALI YATAKIWA KUANGALIA UPYA MFUMO WA ELIMU

WIZARA ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, imeombwa na serikali za
wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuangalia upya mfumo wa elimu ya juu
hapa nchini wakidai kuwa unaegemea zaidi elimu ya darasani, ambayo
haiwajengi katika kujiamini na kushindana katika soko ya ajira.
Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na viongozi wa wanafunzi wa vyuo
vikuu katika mkutano wa muungano wa serikali za wanafunzi wa vyuo
hivyo  kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,
uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela mkoani hapa.
Paul Makuri ambaye ni Makamu Rais wa Muungano huo, alisema wanafunzi
wanapokuwa vyuoni nchini, hawapati nafasi ya kutembelea wanafunzi wa
vyuo vingine na kujifunza wanavyoandaliwa kushindana, katika soko
baada ya kuhitimu masomo.
Alisema utakuta mwanafunzi anamaliza chuo hajawahi hata kutoka nje
hata ya chuo, kukutana na wanafunzi kutoka maeneo mengine hususan
katika nchi za jirani, ambazo zinasifika kwa wahitimu wao kukubalika
katika soko la ajira.
“Mfumo uliopo hapa kwetu umejielekeza zaidi katika elimu ya darasani
tu, hali ambayo inamkosesha mhitimu uwezo wa kujiamini, katika
kujieleza mbele ya watu na kuoeneka hajui au ni dhaifu, katika ujuzi
wa mambo,” alisema.
Aidha aliongeza kuwa wanafunzi hawapati fursa za kutembelea
vyuovingine au maeneo mbalimbali, kuona watu wa jamii na nchi tofauti
wanavyofanya mambo yao na kujifunza kujiamini.
Alisema uwezo wa kujiamini ni changamoto kubwa nchini, kutokanana
mazingira halisi ya utoaji wa elimu ulivyo, hali iliyofanya wahitimu
wa vyuo vikuu  kukosa ajira, sababu ya kuonekana katika mazoezi ya
usaili, kuwa hawajiamini na kuwadharau kuwa hawawezi kuleta tija
katika taasisi waazoomba ajira.
Akizungumzia malengo ya mkutano huo wa serikali za vyuo vikuu, kutoka
nchi za Afrika Mashariki ni kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali,
yanayowakabili vijana wasomi katika nchi hizo, pamoja na uchaguzi wa
viongozi wa Muungano huo kwa kipindi kijacho.
Alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa umoja huo, ni kuwawezesha vijana
hao wasomi kushiriki katika masuala muhimu katika mtengamano wa Afrika
Mashariki.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post