Kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi mpinga (Kushoto) akipokea Tshirt kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayofanyika kitaifa mkoni Iringa ambapo Airtel ni wadhani wakuu. makabithiano hayo yalifanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarni jijini Dar es saalam. akishuhudia ni Mkaguzi msaidizi wa polisi inspector Deus Sokoni, madhimisho ya wiki ya Usalama barabarani yanaanza leo jumatatu.
Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akizungumza na maasa wa polisi mara baada ya kukabithi Tshirt ambazo zimebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria” zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani nchini nzima. Kulia ni Kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi mpinga akifatiwa na Mkaguzi msaidizi wa polisi inspector Deus Sokoni na kushoto ni Mratibu msaidi wa polisi Bonaventura Nsokolo.
Mfanyakazi wa Airtel bwana Gregory Ndenyishau akishusha box lenye Tshirts ambazo zitatumika katika wiki usalama barabarani katika ofisi za makoa makuu ya polisi wa usalama barabarani jijini Dar esa saalam ambapo Airtel ni wadhani wakuu wa kampani ya usalam barabarni kwa mwaka huu, akipokea ni Mratibu msaidi wa polisi Bonaventura Nsokolo.
Airtel yakabidhi Fulana zenye Ujumbe maalum kwaajili ya kuhamasisha usalama barabarani
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua na kudhibitiwa.
Wiki ya nenda kwa usalama barabarani inafunguliwa kitaifa mkoani Iringa katika viwanja vya Samora kuanzia tarehe 17-22 mwezi Septemba ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MHE. DKT. EMMANUEL NCHIMBI kwa niaba ya Mh, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na wakati wa hafla maalum ya makabidhiano ya Fulana Ofisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema "Airtel tunaona ni haki na ni sawa kuendelea kuthamini usalama barabarni na tunayo dhamira thabiti ya kuhakikisha tunaelimisha na kuhamasisha jamii na waendesha vyombo vya moto kuzingatia na kutii sheria za usalam barabarani, hivyo basi tunaomba watanzania kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha kwamba vyombo vya moto zinakaguliwa na kubandikwa stika maalumu za nenda kwa usalama barabarani"
Airtel inadhamini kampeni hii kwa miaka 4 mfululizo ambapo mwaka huu mbali na kuchapisha stickers imejitolea fulana 800 zenye thamani ya Tsh 8 zilizo na ujumbe maalumu kwa mwaka huu usemao“ Pambana na ajali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria” makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarini jijini Dar es saalam.
"Airtel Tanzania imeamua kuunga mkono kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa sababu ya ongezeko kubwa la ajali za barabarani ambazo zinaathiri wateja wetu, aliongeza Bi Mtinde
Bado Airtel haitaishia hapo tayari tumeshajipanga kufanya kampeni mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa waenda kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kupunguza ajali barabarani huku tukishirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani. alimaliza kwa kusema.
Nae kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani Mohamedi Mpinga alisema "Ninawashukuru sana Airtel kwa ushirikiano wenu katika mkakati wetu wa kupunguza ajali barabarani, hadi sasa maandalizi yote ya wiki ya nenda kwa usalama yamekaa sawa na nawahamasisha sana wananchi wote wajitokeze katika vituo vyetu vyote nchini ili waweze kukagua magari yao na kujipatia stika za usalama barabarani
Kwa mkoa wa Iringa ambapo ndiko tunafanya maadhimisho ya Usalama barabarani pia tutafanyia ukaguzi pale katika viwanja vya Samora vilevile kituo cha polisi kati maeneo ya sokoni, kituo cha checkpoint ivumbilo na kile cha mafinga, alimaliza kwa kusema Kamanda Mpinga.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia