BREAKING NEWS

Sunday, September 16, 2012

WATUMISHI FLYING CARGO ARUSHA WAUSHUTUMU UONGOZI WA KAMPUNI HIYO

BAADHI ya watumishi katika kiwanda cha Flying Cargo kilichopo Mbauda jijini Arusha wameulaumu uongozi wa kampuni hiyo kwa kuwadhalilisha na kuwapunja madai yao mbalimbali  huku wakiitaka serikali iwatupie jicho wawekezaji hao.

Kiwanda hicho kinajishughulisha na biashara ya kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi ambapo kwa sasa kinamilikiwa na watanzania wenye asili ya kiasia.

Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya watumishi hao walisema ya kwamba baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo hususani wenye asili ya kiasia huwadhalilisha kwa kuwatukana matusi ya nguoni bila kujali umri wa mtumishi yoyote.

Walisema kwa nyakati tofauti ya kwamba baadhi yao ambao ni madereva wa malori huenda safari ndefu nje ya nchi  na pindi inapotokea ajali yoyote hukatwa mishahara yao yote na marupurupu kwa sababu zisizoeleweka.

Bila kutaja majina yao hadharani kwa kuhofia kutimuliwa kazi walidai kwamba kumekuwa na tabia ya upendeleo kwa baadhi ya watumishi ambao huletwa na vigogo kutoka serikalini na wale waliokuja kutafuta kazi kivyao kitendo ambacho kimepelekea kuibuka kwa tabia ya upendeleo.

“Sisi madereva tunaokwenda safari ndefu endap ikitokea ajali yoyote njiani hawa wamiliki hawatambui hilo ukirudi wanakukata mshahara na pesa yako yote bila sababu za msingi”walisema watumsihi hao

Hatahivyo,walibainisha kwamba uongozi wa kampuni hiyo umekuwa ukiwatumia kutoa ushahidi kwa kampuni za bima pindi wanapopatwa na ajali na mara wakishalipwa fedha za ajali hizo wao hutimuliwa kazi bila kupewa chochote.

“Hii kampuni inajali maslhai yake na siyo maslahi yetu kwa mfano dereva unapopata ajali wanakutumia kutoa ushahidi kwenye kampuni ya bima na mara wanapolipwa wewe hawakujui hii si sawa kabisa”walisisitiza watumishi hao

Kufuatia madai hayo gazeti hili lilimtafuta juzi mkurugenzi wa kampuni hiyo,Parbat Sisodiya ambapo alikanusha  madai hayo na kusema kwamba madai hayo hayana ukweli wowote.

Akihojiwa na gazeti hili ofisini kwake alisema kwamba  madai ya matusi ni uongo mkubwa kwa kuwa endapo mtumishi akitukanwa ana haki ya kufikisha madai yake kwenye vyombo vya dola.

Kuhusu madai ya kupunjwa mafao yao mbalimbali ikiwemo mshahara alijibu kuwa kuna baadhi ya madereva wamekuwa wakiuza mafuta ya dizeli na petrol wawapo safarini na pindi wanapogundulika hukatwa posho zao za safari kufidia pengo hilo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates