MBUNGE wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joshua Nassari, ameshikilia msimamo wa kupiga marufuku Mwenge wa Uhuru kufika jimboni kwake na kuwataka wananchi kuupuuza akidai hauna tija kwa
maendeleo yao.
maendeleo yao.
Aliwataka wananchi jimboni humo wakae mkao wa kula kwani jitihada za kuyatwaa mashamba makubwa yanayomilikiwa na wageni, zinaendelea hivyo wawe wavumilivu.
Bw. Nassari aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara uliofanyika kwenye Kata ya Usa River, wilayani humo.
Aliwaataka wananchi kuupuuza mwenge huo, kutoshiriki kuchangia mchango wowote na kusisitiza kama mtu yeyote atabughudhiwa kutokana na ujio wa mwenge amualifu.
“Sioni sababu ya Mwenge wa Uhuru kukimbizwa maeneo mbalimbali nchini kwani badala ya kuhamasisha maendeleo, umegeuka sehemu ya ufujaji wa fedha za wananchi.
“Hali hii inachangia umaskini wa Taifa na kuhamasiha maovu katika maeneo yote ambayo mwengu huu unalala, nasema hivi, Mwenge wa Uhuru marufuku kufika jimboni kwangu.
“Mtu yeyote ambaye ataombwa mchango kwa ajili ya mwenge muiteni mwizi na mimi nitakuwa wa kwanza kuuzima baada ya kufika jimboni kwangu,” alisema Bw. Nassari.
Aliwataka wananchi hao kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao kisiasa na kuihadharisha Halmashauri ya Meru kuzingatia maadili ya utendaji kazi na kuacha kuwabughudhi wananchi kwa kuwachukulia bidhaa zao hasa wanapokusanya ushuru sokoni kupitia wakala wao.
Ally Abeid huenda kuna siku akatangaza hata kuichana bendera ya nchi au kuvunja ile nembo ya Taifa na mwisho wake ule wimbo wa Taifa atasema ni mrefu sana
ReplyDeleteTuesday at 6:00pm · Like
Joshua Sikawa Mi mwenyewe siufagili kabisa coz 2nachangishwa fedha 2!! nibora uwekwe makumbusho kama 2nashida 2kauangalie pale.
Tuesday at 6:22pm via mobile · Like
Mukhtar Abdul Bolyao Huyo Mtoto ana Kichaa. Hata kama huupendi huna lakufanya subifi 2015 ikiwezekana. Hata mimi si fagilii Gharama zinazo tumika Kutembeza Mwenga,ukilinganisha na faida zake. But you c...See More
Tuesday at 7:07pm · Like
John Toto Rufomoka Mi nilisha shauri katiba ijayo hawa wagombea wawe wanapimwa akiri kwanza kabla ya kuteuliwa kugombea na chama chake,hivi ARUSHA nani amewaloga hata mkashindwa kupata viongozi wakuwawakilsha .
Tuesday at 10:41pm · Like
Ernest Josephat daa kweli hauna maana make ni garama 2 una leta kama vipi wa upeleke makumbusho kama mtu hana shida nao akahuone sababu hauna tena tija kwetu