Kamati ya Usaili ya uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Arusha (ARFA)imetupilia mbali pingamizi dhidi ya wagombea wawili wa nafasi ya mwenyekiti na katibu na mmoja wa nafasi ya uwakilishi wa vilabu aende na maji .
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya usaili wa waliomba nafasi mbali mbali katibu wa kamati hiyo John Bayo alisema kuwa kamati yao imewasaili wagombea wote na kuwa wagombea hao wote wamepitishwa na kamati hiyo isipokuwa watatu wametakiwa kuwasilisha vyeti halisi kabla ya tarehe 21.
Bayo alisema kuwa wamewapa nafasi kuleta vyeti kwa kuwa hapa mkoani wapo kikazi na kuwa wagombea hao wameviacha kwenye mikoa ambayo ni makazi yao ya kudum.
''Maamuzi yetu haya tuliyoyatoa ni ya muda kufuatia agizo tuliopewa na TFF kuwa tupeleke nakala haraka iwezekanavyo iliwapeleke NECTA kwa ukaguzi zaidi kwani sisi tumeviona kwa macho lakini baraza ndio wana kumbu kumbu zote''alisema Bayo
Bayo alisema kuwa baada ya usaili huo wagombea watajulishwa kuwa wanagombea kwa nafasi ipi ikufanikisha zoezi hilo la usaili.
Alisema kuwa kamati yao ilipelekewa pingamizi 3 kwa nafasi ya mwenyekiti na katibu lakini hawa kuona ushahidi wa kisheria kwenye pingamizi hizo hivyo walitupilia mbali pingamizi hizo dhidi ya wagombeoa hao ila nafasi moja pingamizi lilifanikiwa.
Bayo alisema kuwa pingamizi dhidi ya mgombea wa nafasi ya uwakilishi wa vilabu Wilclify Keto walitumia katiba ya Tff ibara ya31 sura ya 2 kwa kuwa mgombea hakuwa mwakilishi wa vilabu kwenye wilaya yeyote hivyo walimuondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
''Kwa ujumla kamati haikuona sababu za msingi kwa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti Khalifa Abdallah Mgonja,na katibu Gerald Munisi kwani waliowasilisha walishindwa kutoa sababu za kisheria mbele ya kamati na badala yake walileta za kinadhaira hivyo walitupilia mbali pingamizi hizo''alisema Bayo
Bayo alisema kuwa tuhuma dhidi ya mgombea wa nafasi ya mwenyekiti zilikuwa 3 na kuziainisha kuwa ni juu ya ubadhirifu haikuwa na ushahidi na nyingine ya utawala haikuwa na sababu za msingi,na pingamizi la mgombea wa nafasi ya katibu zilikuwa 2 ya kwanza ilisemekana hana elimu ya kidato cha nne lakini mgombea aliwasilisha vyeti halisi na pingamizi la pili hakuwa na haiba na uadilifu waliona yote hayakuwa na ushahidi hivyo waliyatupilia mbali.
Pingamizi dhidi ya mgombea wa uwakilishi wa vilabu liliwekwa na omary walii kwa kusema kuwa mgombea hakuwa mwakilishi wa vilabu kwenye wilaya yeyote kama katiba ya tff ibara ya 31 sura ya pili linavyosema kuwa muwakilishi wa vilabu ngazi ya wilaya ndiye mgombea halali wa nafasi ya uwakilishi kwenye ngazi ya mkoa wagombea kwenye nafasi hiyo walikuwa wawili.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia