mkurugenzi wa mfuko wa hifadhi ya jamii LAPF Eliud Sanga katikati akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya mkutano wao wa mwaka ambao unatarajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa simba ulioko katika jengo la kimataifa la mikutano AICC mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na waziri wa TAMISEMI ofisi ya waziri mkuu Hawa ghasia na kufungwa na mh,Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya kikwete
ZAIDI ya wanachama 400 wa mfuko wa jamii wa LAPF pamoja na wadau mbalimbali wa mfuko huo wanatarajiwa kuuthuria mkutano wa tano wa mfuko huo unatarajiwa kufanyika jijiji Arusha .
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa mfuko huo Eliud Sanga alisema kuwa mkutano huo ni watano kufanyika tangu kuanzishwa kwa mfuko huo na hii ni mara ya kwanza kufanyika jijini Arusha.
Alibainisha kuwa zaidi ya wanachama 400 wanatarajiwa kushiriki mkutano huu pamoja na wadau mbalimbali wa mifuko ya jamii wakiwemo wa ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi huku akibainisha nchi mbalimbali zinazoshiriki mkutano huu ni pamojna na wadau wa mifuko ya jamii kutoka nchi za zilizopo katika jumuiya ya Afrika mashariki ambapo alitaja kuwa ni pamoja na kenya ,uganda ,burundi Rwanda na zambia.
Alisema kuwa kwa Apa watu wengine ambao watashiriki na wamealikwa katika mkutano huu ni pamoja na shirika la nyumba tanzania halimashauri vingozi wa halimashauri zote hapa nchini ,meya wa halmashari zote ,makatibu tawala pamoja na mifuko mingine ya kijamii.
Alisema kuwa katika mkutano huu kutakuwa na mada mbalimbali ambazo zitajadiliwa na washiriki ikiwemo mchango wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii, Nafasi ya mufuko wa jamii ,kujiandaa kustaafu pamoja na kuwapa washiriki elimu kuhusiana na ugonjwa wa saratani.
Alisema leongo la mkutano huu ni kupanua wigo wa maoni pamoja na mawazo ya wananchama huku akibainisha kuwa kauli mbiu ya mkutano huu kwa mwaka hu ni hifadhi ya jamii na ukuaji wa uchumi,
Alisema kuwa mkutano huu utafanyika kwa siku mbili ambapo alibainisha kuwa unatarajiw akufunguliwa na waziri wa tamisemi ofisi ya waziri mkuu na kufungwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.