MACHINGA ARUSHA WAVAMIA ENEO LA WAZI

Wanawake wakiwa wanalinda maeneo yao huku wengine wakiendelea kujigawia



KUNDI la wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama (Wamachinga) jijini
hapa, wamevamia eneo la la wazi lililopo Ngarenaro na kujigawia maeneo
tayari kwa kufanya biashara.
Kundi hilo la Wamachinga limevamia eneo hilo ambalo lilikuwa
limezungushiwa mabati  kwa kipindi cha muda mrefu kilichopo ngarenaro
jijini hapa wakidai kuwa eneo hilo ni la serikali hivyo wanaenda hapo
hapo kufanyia biashara maana wao wenyewe ni serikali tosha.
NIPASHE lilifika eneo la tukio lilishuhudia wananchi hao wakiwa
wanajigawia sehemu za biadhara huku wengine wakiwa wameanza kuchimba
kwa ajili ya kujenga vibanda vyao.
Wakizungumzia  tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara hao walisema
wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na kukosa sehemu za  kufanyia
biashara kwani eneo walilopewa la uwanja wa NMC Ltd  ni dogo na
haliwatoshi.
Mmoja  wa wafanyara hao aliyejitambulisha kwa jina la Emanuel Mushi,
alisema wao wamechukua hatua hiyo kutokana na kitendo cha kukosa eneo
la kufanyia biashara katika kiwanja cha NMC  huku mkandarasi ambaye
amepewa tenda hiyo ya kuwagawia maeneo akiwa anawazungusha.
Aidha alisema wameamua kufanya au kuchukua hatua hii ili serikali ijue
wamachinga Arusha hawana mahala pa kwenda na wawatafutie sehemu ya
kuwaweka ili wafanyie biashara zao.
Alisema wamesubiri kwa muda mrefu na tangu waambiwe wanagawiwa eneo
hilo hawajapatiwa na wamekuwa wakizungushwa tu bila ya mafanikio
yoyote hali ambayo inawafanya wao kuishi kama ndege.
“Leo asubuhi sisi tuliokuwa tumeweka vitu vyetu hapa nje ya soko la
Ngarenaro tumefukuzwa kama mbwa na mbaya zaidi wametufukuza wakiwa
hawajatupa sehemu ya kwenda, wanatupelekapeleka na tulivyoona hivyo na
ili eneo tunaliona wazi kila siku,  tukaamua kuvamia ili tukae hapa,”
alisema Rosemary Mollel.
“Unajua eneo lile ni dogo kwa kweli ni robo ya Wamachinga tu ndio
wameingia katika eneo lile kibaya zaidi,  askari wanatufuata
tukiwauliza tuende wapi wanasema mtajua wenyewe kila tukaapo
wanatufukuza kibaya zaidi wanatuambia kuwa swali kama hilo msiniulize
maana wakati mnakuja kutoka vijijijini kwenu hamkututaarifu kwakua
mlikuja kimnya kimnya basi ondokeni ivyo ivyo kama ulivyokuja,”
alisema Lucas Seneu.
“Serikali imekuwa ikifanya kazi kwa kuwakomoa kwani wanadhani
wamachinga wengi ni Chadema,  hivyo, wanavyofanya hivi wanatukomoa,
kitu ambacho sio  kweli,” alidai.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post