MFANYABIASHARA mwenye asili ya kiasia ambaye pia ni mmiliki wa kiwanda cha Auto Electric Co ltd kilichopo Njiro jijini Arusha(jina limehifadhiwa) amewatimua waandishi wa habari ofisini kwake waliofikakuchunguza madai ya kujenga ukuta pembeni mwa barabara kuu iendayo Mbauda.
Mbali na tukio hilo pia alimfokea vikali mlinzi aliyewafungulia lango la kuingilia kiwandani hapo kwa kitendo cha kuwafungulia waandishi hao kuingia kiwandani kwake.
Hatua hiyo imefuatia mara baada ya waandishi wa habari akiwemo wa gazeti hili kupata taarifa ya ziara ya viongozi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha iliyotembelea eneo la Kambarage kuchunguza madai ya kiwanda hicho kujenga ukuta karibu na barabara kuu iendayo Mbauda.
Taarifa zinadai kwamba timu ya wataalamu wa ujenzi na mpango miji ilifika eneo hilo na kisha kupima umbali wa ukuta huo na kisha kubaini ya kwamba kuna ukiukwaji mkubwa wa ujenzi huo.
Taarifa hizo kutoka kwa baadhi ya watumishi wa manispaa hiyo zindai kwamba ukuta huo ulijengwa umbali wa mita 48 badala ya 60 kitendo amabcho kinyume cha sheria.
Mara baada ya taarifa hizo kuwafikia waandishi wa habari waliamua kutembelea kiwandani hapo na mara baada ya kuwasili walijitambulisha na kisha kufunguliwa lango la kuingilia kiwandani hapo.
Lakini walipowasili eneo la mapokezi na kisha kuulizia uongozi wa kiwanda hicho ndipo alipojitokeza mwanamke mmojawapo na kutamka kwamba yupo mmiliki wa kiwanda hicho lakini hawezi kuzungumza na waandishi wa habari.
Wakati wa majibishano ndipo alipojitokeza mmiliki huyo na kuwauliza waandishi kwamba wanataka nini na baada ya kuelezea shida yao ndipo alihoji kwa kuwauliza ya kwamba walipitia njia gani kuingia kiwandani hapo.
“Mmeingiaje humu nani kawafungulia geti nawauliza je mmeingiaje humu ndani”aliwahoji waandishi wa habari huku akielekea kwa mlinzi aliyewafungua lango la kuingia kiwandani hapo
Hatahivyo,alipobanwa ajibu madai ya kujenga ukuta karibu na barabara kuu mmiliki huyo alisema kwamba hawezi kujibu maswali hayo na kutaka waulizwe watumishi wa manispaa ya jiji la Arusha.
Alisema kwamba yeye siyo mjinga hadi ajenge ukuta huo uliodumu kwa miaka mingi bila kufuata sheria za mipango miji na wakati akiendelea aliwataka waandishi watoke nje ya kiwanda hicho.
"Mnadhani mimi ni mjinga huu ukuta sikujenga jana wala juzi ni ukuta wa muda mrefu sitaki kuhojiwa nendeni manispaa kwanza naoma mtoke mje tokeni haraka"aliwafokea waaandishi wa habari hao
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia